WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi
wa kabichi: Hawa ni viwavi wenye rangi ya kijani na alama ya
mstari wa kung’aa mgongoni. Nondo hutaga mayai chini ya jani na baada ya
kuanguliwa viwavi hawa hula sehemu ya chini ya jani na kucha ngozi nyembamba
mfano wa dirisha la kioo. Ni muhimu kuwadhibiti viwavi hawa kwa sababu ndio
wanaoleta madhara makubwa. Viwavi wa kabichi huzuiwa kwa kunyunyizia moja ya
dawa zifuatazo:- Nogos,
Permethrin,Dimethoate, Sevin W.P. na Sumicidin.
Nzi wa Kabichi: Mashambulizi hufanywa na kiluwiluwi
mwenye rangi ya kijani au bluu. Hula majani yote ya kabichi na kubakisha vena
au vishipa vya majani. Inzi wa kabichi wanaweza kuzuiwa kwa kutumia dawa za Sevin, Dimethoate, Permethrin na
Fenvalerate(sumicidin)
Sota: Hawa ni funza wakubwa wenye
rangi ya kijivu. Hupendelea kujichimbia katika udongo wakati wa mchana na
kukata miche michanga karibu na usawa wa ardhi wakati wa usiku. Zuia wadudu
hawa kwa kutumia majivu au dawa kama vile Carbaryl,
Fenvalerate au Decis mara baada ya kuotesha. Kama mche utakatwa, mtoe mdudu
huyu kwa kumfukua na kumuua. Kisha pandikiza mche mwingine.
Vidukari au wadudu
mafuta: Wadudu hawa ni wadogo sana wenye rangi ya
kijani, nyeusi au khaki. Baadhi yao wana
mabawa na wengine hawana. - Hufyonza utomvu wa mimea na husababisha majani
kubadilika rangi na kuwa meupe au njano iliyopauka. Mmea hudumaa na hatimaye hukauka. Zuia kwa
kunyunyiza mojawapo ya dawa hizi Fenvalerate,
Dimethoate, Karate, Nogos.
Minyoo Fundo: Ni minyoo wadogo wanaoishi ardhini
na ambao hawaonekani kirahisi kwa macho. Hushambulia mizizi na kusababisha
kabichi kudhoofu na kushindwa kufunga vizuri. Mimea iliyoshambuliwa, mizizi
yake huwa na nundunundu. Kuzuia: Matumizi ya mbolea za asili kila msimu
husaidia kupunguza kuzaliana kwa wadudu hao. - Tumia mzunguko wa mazao,
usiotesha zao la jamii ya kabichi baada ya kuvuna kama vile kabichi ya kichina,
koliflawa,n.k Otesha mboga kama vile karoti, radishi, vitunguu au mahindi. -
Ondoa masalia yote shambani ambayo yanaweza kueneza wadudu hawa na yachome
moto.
MAGONJWA
Kuoza shingo; Husababishwa na vidudu vya bacteria
ambavyo viko kwenye udongo. Hushambulia kabichi na kuzifanya zibadilike rangi. Kuoza na kutoa harufu mbaya. Vidudu vidovidogo
huonekana pia kwenye sehemu iliyooza. Kuzuia:
·
Epuka
kujeruhi kabichi wakati wa kuvuna.
·
Vuna
kabichi wakati hakuna mvua - Usilundike kwa wingi na kwa muda mrefu.
·
Hifadhi kwenye sehemu yenye ubaridi na hewa ya
kutosha.
·
Ng’oa
masalia, choma moto na lima shamba mara moja baada ya kuvuna - Tumia mzunguko
wa mazao.
Uozo Mweusi; husababishwa na Bakteria . Majani hugeuka kuwa
njano na baadaye kuwa kahawia . Majani huanza kunyauka kutoka kwenye kingo zake
na kuacha alama ya “V” yenye rangi nyeusi isiyokolea. Baadaye majani hunyauka na kupukutika. Kama
ukikata jani au shina, mviringo mweusi huonekana kwenye vena.
Kuzuia:
·
Badilisha
mazao.
·
Usipande
kabichi au jamii yake kwa muda wa miaka 2 kwenye eneo lililoadhirika.
·
Otesha
kabichi kwenye sehemu ambayo haituamishi maji.
·
Kitalu na mazingira yake viwe safi daima.
·
Punguza
miche ili kupunguza msongamano.
·
Ondoa masalia yote baada ya kuvuna ya yachomwe
moto.
·
Otesha
mbegu zilizodhibitishwa na wataalam.
Kuoza shina; Ni ugonjwa
waukungu, Madoadoa yaliyodidimia yenye rangi ya kahawia huonekana kwenye shina
karibu na usawa wa ardhi, ikifuatiwa na kuvimba kwa shina. Baadaye uyoga mweusi huonekana kwenye uvimbe
huo. Uozo wa rangi ya kahawia huonekana ndani ya shina. Majani huwa na madoa meusi ya mviringo
yaliyozungukwa na uyoga mweusi.
Kuzuia:
·
Otesha
kabichi sehemu ambayo haituamishi maji.
·
Badilisha mazao, usioteshe kabichi kwenye eneo
lililoathirika kwa muda wa miaka 3.
·
Lima shamba mara baada ya kuvuna ili kuwezesha
masalia kuoza haraka kabla ya kuotesha tena.
·
Ondoa kabichi zote zilizoshambuliwa shambani.
·
Tumia
dawa ya kuzuia ukungu kama vile Ridomil.
Uvimbe wa mizizi; Husababishwa na
ukungu. Hushambulia mizizi na dalili zake ni kudumaa kwa mmea na majani
kukunjamana . Baadae mmea huoza
Kuzuia:
Badilisha mazao shambani.
Madoa Meusi: Chanzo ni ukungu. Majani huwa na madoa madogo
madogo ya mviringo yenye rangi ya njano . Baadae madoa huwa makubwa na hugeuka kuwa
meusi.
Kuzuia:
·
Badilisha
mazao
·
Hakikisha shamba ni safi wakati wote
·
Ikibidi tumia dawa za ukungu kama vile
Kocide,Cupro, n.k. ·
·
Ubwiri
Vinyoya: Ni ugonjwa wa ukungu. Hupendelea hali ya
unyevunyevu na baridi kali. Huanzia kwenye kitalu . Mabaka ya mviringo yenye
rangi ya njano huonekana upande wa juu wa jani. Baadae hubadilika na kuwa rangi
ya zambarau iliyochanganyika na nyeupe upande wa chini wa majani.
Kuzuia:
·
Tumia
mzunguko wa mazao.
·
Hakikisha
udongo hautuamishi maji na kitalu ni kisafi wakati wote.
·
Tumia za ukungu kama Zineb, Didhane, M45,
Kocide, Topsin-M na Ridomil.
Kuoza shina au
Kinyaushi: Husababishwa
na ukungu. Hushambulia miche michanga. Miche iliyoshambuliwa huonyesha dalili
za kukauka. Miche mikubwa huonyesha dalili za kudumaa. Sehemu ya shina iliyo
karibu na ardhi hulainika na kuwa rangi ya kahawia.
Kuzuia:
Punguza
miche kama imesongamana. Nyunyiza dawa ya ukungu Kama Didhane M-45, Ridomil,
Topsin-M.
0 comments:
Post a Comment