Friday, August 12, 2016

FAHAMU KILIMO BORA CHA MATIKITI MAJI


Tikiti maji ni mboga/tunda linalolimwa hasa katika maeneo ya joto lenye kiwango cha joto cha 22-28 0c na mvua 600 - 400mm kwa mwaka. 
Matikiti yanahitaji hali ya hewa yenye joto na mwangaza wa jua wa kutosha . Kiwango kidogo cha unyevu kwa sababu unyevu mwingi unasababisha maradhi.  Unyevunyevu    mwingi unaadhiri ubora na utamu wa tunda. Vilevile, yanastawi vizuri katika aina mbalimbali za udongo wenye rotuba ya    kutosha na wenye kupitisha maji vizuri.

Aina  za matikiti maji


 NEGRA F1

Aina hii ya matikiti maji ni ya  mviringo yenye mazao na sifa nzuri”
Ubora wake
 • Yana mazao mazuri, na uwezo wa kukupa tani 46 kwa kila ekari
• Ni matamu sana na yenye wekundu wa kung’ara
 • yanakomaa katika muda wa siku 100-120
• Ni mviringo na yenye rangi ya kijani kibichi na hutoa matunda yenye  mizani kati ya kilo 7-10
 • Mmea hukua haraka na una mazao mazuri
 •Yamezungukwa na nyama ngumu, nzuri, yenye kukuwezesha  kusafirisha hadi sehemu za mbali
 • Yana kinga dhidi ya  ugonjwa wa mnyauko unaosababishwa na  vimelea aina ya Fusari (Fusarium wilt)

SENTINEL F1 


  ni aina mpya ya matikiti ya mviringo marefu” 
Ubora wake

• yanaweza kuzaa sana hadi tani 50 kwa kila ekari
• Ni marefu, yameshiba na yana rangi ya pundamilia
 • ni tamu, yan wekundu uliokolea na nyama iliyo na maji mengi
 • Yanawezakutoa matunda ya kufanana na yaliyo na uzani kati kilo 11 - 14
• Matunda yana nyama nyingi na umbo inayokuwezesha kusafirisha masafa marefu
 • yana kinga dhidi ya maradhi ya vimelea aina ya Fusari (Fusarium wilt Race 1)
 • yanakua tayari katika muda wa siku 100 -120 
Mbali na kuwa na faida mbali mbali kiafya tikiti maji linaweza kumtoa mkulima wa kawaida katika umaskini. Hii kutokana na sababu zifuatazo.
·   Tikitimaji ni zao la bustani linalochukua miezi 3-4 kuvunwa, hivyo kwa mwaka linaweza kuvunwa mara 3 hadi 4
·         kwa ekari moja mavuno ya tikiti maji ni matunda 2000 - 8000  au zaidi kwa miezi 3-4 kutokanana uangalizi wa mkulima katika shamba ikiwa ni kutumia mbolea kama inavyo takiwa, kuzuia wadudu na magonjwa, n.k. Pamoja na nafasi iliyotumika katika upandaji (1x1m, 2x2m, 1.5 x 1.5m).

JINSI YA KUJUA FAIDA

Katika maeneo mengi ya Tanzania bei ya tikiti maji lenye sifa nzuri ni shilingi 2,000/= hadi 3,000/=
kwa bei ya 2,000/= na mavuno ya 2000 matunda/ekari (Matunda mazuri)
Baada ya mavuno utajipatia kiwango cha chini kisichopungua jumla ya Tsh.4,000,000/= kwa mwaka ni 12,000,000/= kwa mavuno ya mara tatu kwa mwaka kwa ekari.

Gharama hii itaenda juu zaidi ama itapungua kutegemea na idadi ya matunda uliyoyapata katika ekari mmoja na bei ya muuzaji. Hivyo unaweza ukapata faida kubwa zaidi ukiongeza uangalizi wa shamba lako na kufuata utaratibu katika ulimaji wa zao hili.

  MAHITAJI

Tikiti maji linahitaji mbolea, maji, kemikali za kuua wadudu na magonjwa pamoja na maandalizi mabali mbali ya shamba ambavyo gharama yake haizidi Tsh. 500,000/= katika uangalizi mkubwa

FAIDA

Hivyo mkulima katika uangalizi wa mzuri ana uhakika wa kupata faida ya Tsh. 3,500,000/=  na zaidi kila baada ya miezi 3-4.  
Ushauri: Kwa mafanikio mazuri na kuinuana kiuchumi wakulima wakiungana na kufanya kilimo bishara watakuwa na nafasi kubwa ya mafanikio kwa maana kiuchumi wanataweza kusaidiana ili kuinua mtaji na kuweza kupata kiasi cha kuanzia shughuli zao za kilimo. 
Share:

2 comments:

  1. asante sanaaa kwa makala yenu

    ReplyDelete
  2. Elimu nzuri sana hususani kwa mtu mwenye lengo la kuwa mjasiriamali kupitia kilimo cha matunda. Hongera kwa kuelimisha umma zaidi juu ya kilimo cha matikiti maji

    ReplyDelete

Blog Archive

Latest Posts

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support