KAMA HUKUSOMA MAKALA ZILIZOPITA BOFYA HAPA KUSOMA ZOTE ILI KUENDELEA
MATUMIZI YA SOLAR POWER SYSTEM HAPA TANZANIA
1. kuzalisha umeme
Asilimia kubwa hapa tanzania hutumia solar kupata nishati ya umeme kwa matumizi ya nyumbani kama kuwasha taa, kuendesha vifaa vya electroniki kama television, friji, kucharge simu na matumizi mengine ya electrobiki. Hii imeweza kusaidia watanzania wengi sana ambao wapo kijijini na kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme hapa nchini kwetu hasa kipindi cha kiangazi. Makampuni ya kichini sasa yamerahisisha maisha kwa kutuletea taa ndogo za kuweka juan yaaan kucharge afu usiku inafanya uangavu safi.
2. Hutumika kwenye vifaa vya electroniki
Pia solar hutumika kwenye vifaa kama vikokotozi (calculator), saa kama kupata power ya kuendeshea sio hapo tuu pia hata redio ndogo zipo zinazotumia solar.
3. Hutumika kwenye taa za kuongozea magari
Mfano halisi hapa kwetu sasa hivi tunatumia solar katika taa za barabaran hasa mikoa kama arusha wanatumia sana na hata ukipita pale pwani kwenye automatic weighbridge(mizani) utaona. Kwa hiyo hakuna tatizo hata umeme ukikatika.
4.Hutumika kupasha joto maji
Hili ni muhimu sana hasa kipindi cha baridi tumeona hii tekinologia ikiwa msaada mkubwa kufanya maisha yanaenda vizuri. Mfano katika vyuo, mahospitali,majumbani na taasisi mbalimbali wameweka huu mfumo ambao umekuwa ukizaa matunda mazuri.
VITU VINAVYOUNDA MFUMO WA KUFUA UMEME KWA MWANGA WA JUA
1. PANEL
Tumeshaona kwenye makala iliyopita aina mbalimbali za panel zinazotumika katika mfumo huu. hiki kifaa kinabadilisha mwanga wa jua kuwa nishati ya umeme kwa kutumia seli ambazo ni silicon. Ni kiungo kikubwa kaitka huu mfumo huu. Panel inatakiwa iwe na uwezo mkubwa kuliko batri unazotumia yaan power yake pia tutaona unaweza ukaunganisha parallel au series hizi panel kutegema matumizi ya umeme wako hata kwa upande wa battery. jinsi ya kuunganisha na kuset kama angle tutaona baadae fuatana nami.
2. BATTERY
Hiki ni kifaa ambacho kina kazi ya kuhifadhi charge na kutumika wakati ambao jua halipo yaani usiku na muda mwingine kipindi cha mawingu. Inashauliwa nguvu ya panel izidi nguvu ya battery. Usijali kuhusu hili kwa kuwa hizi nguvu huwa zinaandikwa kwenye kifaa chenyewe kwa hiyo ni kuangalia tuu unafahamu vizuri mfano 80W.
3. INVERTOR
Hiki ni kifaa kinachotumika kubadilisha aina ya umeme unaozalishwa na panel yaan dirct current (dc) kwenda alternating current yaani (ac) kwa matumizi. Pia kama tulivyoona kwenye panel na batri hata inveta inatakiwa ifananane kiuwezo na battery yako au hata ikizidi sio mbaya lakini isiwe na uwezo mdogo kuliko battery yako.
4. CHARGER CONTROLLER
Hiki ni kifaa muhimu sana katika mfumo huun Ambacho hutumika kurekebisha kiwango cha charge kinachofikia battery yako kuzuia overcharge na kupungua kwa uimala wa battery yako. Hiki kifaa kinaunganisha kati ya panel na battery na invertor kwa ajili kuonyesha alama kuwa battery limejaa na inazuia kuendelea kuchajiwa na panel yako. Pia unaweza ukatumia direct current kwa taa maalumu za solar kama 8A,2A na zinginezwe.
5. WIRES
Hizi zinatumika kama kuunganisha mzunguko wa umeme kutoka kwenye panel kupitia vifaa vyote hadi kwenye matymizi ya mwisho ya mtumiaji. Pia kunatakiwa kuwa na uangalifu hapa kwa sababu huu ni sawa na umeme wa tanesco kwa hiyo sheria za uunganishaji ni zile zile hasa kama ukubwa wa nyaya kwenye socketi,switch,taa,kutoka kwenye panel, batery na pengine yaani wire ring tutaona baadae endele kufuata nami msomaji.
6. VIFAA VINGINE
Hapa ni muunganiko wa vifaa ambavyo vinawezesha mfumo kukamilika kama bulib,switch,socket breaker,main switch na vingine vingi tutaviona kwenye jinsi ya kuunganisha huu mfumo mzma ndungu msomaji endelea kufuatana nami.
TAHADHARI YA KUCHUKUA UNAPONUNUA VIFAA HIVI
- panel inatakiwa iwe na uwezo wa kuzalisha kiwango unchokiitaji ktokana na matumizi
- Power ya battery isizidi kiwango cha panel yako kama tulivyoona juu
- kuwa makini na aina na ukubwa wa nyaya recommended
- Kupata ushauri wa mtaalamu kabla ya kununua vifaa hivyo vyote kama panel na vingine
- Kuzingatia brand ya watengenezaji yaan kampuni lililotengeneza kulingana na uchumi wako mfano ni bora upoteze pesa nyingi ununue kifaa kizuri kinachodumu.
FAHAMU JINSI SOLAR ITAVYOMALIZA TATIZO LA KUKATIKA KWA UMEME
Solar system inauwezo wa kumaliza tatizo hili kama serikali ikiwekeza katika hili. inauwezo wa kuchangia kiwango kikubwa cha umeme katika grig ya taifa kama ilivyo gesi asilia. Pia katika famili level kama kukiwepo na mfumo wa automatic redirection yaan kama umeme ukikatika unajiwasha umeme wa solar na kuendelea na matumizi yetu ya kawaida. kwa hiyo kuna iprovement inaitajika katika hili hasa kwenye majumba ya biashara wengi wanatumia generetor kwa gharama kubwa wakati ana uwezo wa kuwekeza katika nishati hii ya bure kabisaa.
MAKALA ITAYOFUATA NI JINSI YA KUUNGANISHA YAANI UFUNDI WOTE UTAKUWA WAZI HAPA KUMSAIDIA MWANANCHI KUJIAJIRI KWA HIYO FUATANA NAMI HUU NI MWANZO KUNA MFULULIZO WA MAKALA NYINGI ZA AINA MBALIMBALI ZINAKUJA KWA HIYO SUPPORT YAKO NDUGU MSOMAJI KUSHARE NA WENZAKO FACEBOOK, WHATSUP, TWEETER NA MITANDAO MINGINE
ITAENDELEA..........................
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI AU KAMA UNA MASWALI UPO FREE KUULIZA KWA AJILI YA KUSAIDIANA ASANTE NDUGU WASOMAJI
solar yangu walt 30 nitumie bettry ngap, maana siuelewi
ReplyDeleteSolar yangu pannel 150 wt na bettery ni N 120 je nipo Sawa hapo na kama Nipo sawa nitumie charger controller ya aina gani? Naomba msaada
ReplyDelete