Wednesday, August 3, 2016

AINA ZA NGURUWE


Ufugaji wa nguruwe hapa nchini umeanza siku nyingi hususani katika mikoa ya nyanda za juu kusini (Mbeya, Rukwa, Iringa, na Ruvuma), Kaskazini (Manyara, Arusha, na Kilimanjaro). Aina za nguruwe wanaofugwa hapa nchini ni wa kigeni, chotara na koo mbalimbali za kienyeji.


Zifuatazo ni aina za nguruwe wanaopatikana hapa Tanzania:-

1.Nguruwe wa Kigeni

  1. large white
  • Asili yake ni Uingereza
  • Ana rangi nyeupe katika ngozi na manyoya
  • Ana masikio yaliosimama, paji la uso lililoingia ndani kama bakuli
  • Ana mwili mrefu mnene
  • Ana tumbo kubwa, mzito na miguu yenye nguvu
  • Ana uwezo wa kukua haraka na kuzalisha nyama isiyo na mafuta akiwa na umri mdogo
  • Ana uwezo mkubwa wa kuzaa watoto wengi kwa mzao
  • Ni mpole na ana uwezo mkubwa wa kutunza watoto
  • Jike ana uwezo wa kutoa maziwa mengi.
Image result for large white

   2.Landrace
  • Asili yake ni Denmark
  • Ana rangi nyeupe na ni mrefu mwembamba
  • Masikio yake ni makubwa na yamesimama kwa mbele na mara nyingi hufunika macho
  • Ana kichwa kidogo na shingo nyembamba ukilinganisha na ukubwa wa mwili
  • Ana uwezo wa kuzaa watoto wengi kwa mzao
  • Ana uwezo wa kukua haraka na kuzalisha nyama isiyokuwa na mafuta mengi
Image result for Landrace

3.Wessex saddleback
  • Asili yake ni uingereza
  • Ana rangi nyeusi na nyeupe mfano wa mkanda kuzunguka mabega na miguu ya mbele
  • Ni mfupi na masikio yameinama kwa mbele
  • Ana mgongo uliopinda mfano wa upinde
  • Ana uwezo wa kutoa maziwa mengi na kutunza watoto.
Image result for Wessex saddleback

4.Hampshire
  • Asili yake ni marekani
  • Ana rangi nyeusi na rangi nyeupe mfano wa mkanda kuzunguka mabega, kifua na miguu ya mbele
  • Ni mfupi na masikio yamesimama
  • Ana mgongo uliopinda kidogo mfano wa upinde
  • Ana uwezo wa kuzaa watoto wengi na kuwatunza.
Image result for hampshire pig

2. Nguruwe chotara

  • Ni uzao unaotokana na kupandisha nguruwe wa aina tofauti kwa mfano nguruwe wa kienyeji akipandishwa na wa kigeni (kisasa)
  • Hustaimili magonjwa ukilinganisha na nguruwe wa kienyeji
Image result for nguruwe chotara

3.Nguruwe wa kienyeji

  • Huwa na rangi tofauti
  • Huwa ni wadogo kwa umbo
  • Hukua taratibu
  • Wana uwezo wa kustaimili mazingira magumu
  • Nyama yake haina mafuta mengi
  • Wana uwezo wa kujitafutia chakula
Image result for nguruwe pori

BAADA YA KUANGALIA AINA ZA NGURUWE ZINAZOPATIKANA TANZANIA MAKALA INAYOFUATA TUTAANGALIA UTUNZAJI BORA WA NGURUWE
Share:

6 comments:

Blog Archive

Latest Posts

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support