Zao la
kabichi hulimwa katika mikoa ya Morogoro, Arusha,Tanga, Iringa, Kilimanjaro na
Mbeya. Kama mboga zao la kabichi lina viini lishe kama chokaa, protini,
kambakamba na maji kwa wingi. Hutumika kutengeneza kachumbari, pia kuchanganywa
na nyama au maharage.
HALI YA HEWA
Zao la
kabichi hupendelea: hali ya ubaridi Mwinuko: Kuanzia mita 1200 hadi 1900 kutoka
usawa wa bahari. Udongo uwe; Tifutifu,
Rutuba nyingi na Unaohifadhi unyevu kwa muda mrefu, Usiotuamisha maji ,
Usio na chumvichumvi nyingi. Kama hauna rutuba ya kutosha ongeza mbolea ya samadi
au mbolea vunde.
AINA ZA KABICHI
Early Jersey Wakefield: Umbo lilochongoka kidogo, Hufunga vizuri, Uzito ni kati ya kilo 1.5 hadi 2.0, Hukomaa mapema siku 90 – 100 tangu kupandikiza.
· Copenhagen Market: Vichwa vya mviringo na hupasuka kirahisi . Hukomaa mapema,
siku 90 – 100 tangu kupandikiza ·
Prize Drumhead: Vichwa vikubwa (kilo 2- 2.5), Vichwa
ni bapa, huchelewa kukomaa (siku 110 – 120) - Huvumulia hali ya jua kali, Pia
vichwa hupasuka. · Oxheart: - Vichwa vidogo huchongoka kama moyo, Hupendwa sana na walaji, Ladha yake ni tamu, hukomaa mapema, Hazina
tabia ya kupasuka. Glory of Enkhuizen: -
Vichwa vya mviringo, Huvumilia hali ya jua kali, Huchelewa kukomaa (siku 110 – 120) na Ina
tabia ya kupasuka.
KUOTESHA MBEGU
Mbegu za
kabichi huoteshwa kitaluni na baadaye huhamishiwa shambani. Andaa kitalu vizuri
na weka mbolea za asili zilizooza vizuri kwa kiasi cha ndoo 5 – 10 za ujazo wa
kilo 20 kwenye eneo la mita za mraba 10. Changanya na udongo kisha lainisha
udongo kwa kuvunja mabonge makubwa kwa kutumia reki. Tengeneza tuta lililoinuka
kwa sentimita 25 na lenye upana wa mita 1.
Mwagilia
maji kwenye tuta siku moja kabla ya kusia mbegu. Kiasi cha mbegu zinazohitajika
ni gramu 1 kwenye eneo la mita 1 ya mraba hivyo hekta 1 huhitaji gramu 200 –
300. Sia katika umbali wa sentimita 15 toka mstari hadi mstari na kina cha nusu
sentimita.Funika mbegu na udongo laini kasha tandaza nyasi kazu ili kuhifadhi
unyevu.Mwagilia maji kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu ziote, huota kwa
muda wa siku 5 – 10.
KUTAYARISHA SHAMBA
Shamba
litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupandikiza.
·
Katua
ardhi kwa kina cha sentimita 30
·
Lainisha
udongo na tengeneza matuta kisha weka
mbolea za asili kwa kiasi cha ndoo 2 kwa kila hatua moja au Mbolea iwekwe kwa
kila shimo kwa kiasi cha kilo kwa shimo.
·
Mbolea ya N.P.K. 5:15:5 yaweza kuwekwa kwa
kiasi cha kijiko 1 cha chai chenye gramu 5 kwa kila shimo.
KUPANDIKIZA MICHE
Miche huwa tayari kupandikizwa shambani baada
ya wiki 3 – 5 tangu kusia mbegu . Miche huwa na urefu wa sentimita 15 – 20.
Ng’oa miche kwa uangalifu na pandikiza kama ilivyokuwa kitaluni na hakikisha
mizizi haipindi wakati wa kupandikiza. Nafasi ya kupandikiza: Hutegemea aina ya
kabichi – zenye vichwa vikubwa (Drumhead) ni sentimita 60 kutoka mche hadi mche
na sentimita 75 toka mstari hadi mstari. – Zenye vichwa vidogo (Oxheart) ni
sentimita 40 – 50 kutoka mche hadi mche na sentimita 60 toka mstari hadi
mstari. – Umbali toka tuta moja na jingine ni sentimita 60. – Muda mzuri wa
kuotesha ni asubuhi au jioni – Baada ya kupandikiza weka matandazo kama vile
nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kuota kwa urahisi.
PALIZI
Zao la kabichi halina mizizi ya kina kirefu
hivyo wakati wa palizi ni muhimu kuwa mwangalifu kwa kupalilia juu juu ili
kuepuka kukata mizizi. Kuongeza matandazo husaidia kupunguza palizi a mara kwa
mara.
UMWAGILIAJI
Kabichi hustawi vizuri zaidi iwapo kuna maji
ya kutosha kwenye udongo. Mwagilia mara mbili au zaidi kwa wiki kutegemea hali
ya hewa na aina ya udongo. Kabichi ambazo hazikupata maji ya kutosha huchelewa
kufunga na huwa na vichwa vidogo. Zikikosa maji kwa muda mrefu na zikapata maji
mengi ghafla, vichwa hupasuka.
MBOLEA
Mbolea ya
kukuzia (S/A) huwekwa baada ya 4 – 6 baada ya kupandikiza miche na kabla ya
vichwa havijaanza kufunga. Kiasi cha kilo 80 huhitajika kwa eka moja. - Kilo 40
ziwekwe baada ya wiki 4 – 6 na kilo 40 ziwekwe tena baada ya mwezi mmoja . Mche
mmoja huhitaji kiasi cha kidogo cha gramu 5. Mbolea iwekwe kuzunguka shina umbali
wa sentmita 10 – 15 kutoka kwenye shina. Muhimu: Epuka kuweka mbolea nyingi,
kwani husababisha vichwa visifunge vizuri (kabichi zinakuwa nyepesi)
KUBADILISHA
MAZAO
Kabichi nizao linalotumia virutubisho vingi
kulinganisha na mboga nyingine,hivyo kabla ya kuotesha kabichi panda mazao
jamii ya mikunde ili kuongeza rutuba. Baada ya kuvuna kabichi otesha mazao
yanayotumia chakula kidogo kama vile karoti, radishi au lettuce. Kubadilisha
mazao pia hupunguza kuenea kwa wadudu waharibifu na magonjwa.
KUVUNA
Kabichi hukomaa katika siku 60 mpaka 210 tangu
kupandikiza miche. Hata hivyo muda wa kukomaa hutegemea aina ya kabichi. Uvunaji
hufanyika kwa kukata shina sentimita 2 – 3 kutoka kwenye kichwa kwa kutumia
kisu. Ondoa majani ya nje na acha majani 2 au 3 ya kijani kwa ajili ya kuzuia
kabichi zisikwaruzike na kuoza wakati wa kusafirisha. Punguza urefu wa majani
ili kurahisisha ufungaji. Ni muhimu uvunaji ufanyike asubuhi au jioni. Ondoa
kabichi zilizooza au kuharibika wakati wa kuvuna, kisha panga zilizobaki
kufuata daraja kama vile ndogo, za kati na kubwa. Mavuno: Kiasi cha tani 40 au
zaidi za kabichi hupatikana kwa hekta moja kama zao limetunzwa vizuri.
HIFADHI
Kabichi ni zao
linaloharibika kwa haraka, hivyo halina budi kutumika mapema iwezekanavyo baada
ya kuvuna. Kabichi kwa ajili ya kuuzwa zisafirishwe mara moja kwa walaji. Kama
usafiri ni mgumu, zihifadhiwe kwenye sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha.
Wakati wa kusafirisha, ziwekwe kwenye matenga au visanduku vya mbao vilivyo na
matundu yanayoingiza hewa ya kutosha. leo tuishie hapa unaweza kuandika
chochote au kutoa ushauri
Nawezaje pata mawasiliano yenu kwa ushauri zaidi
ReplyDeletesincan
ReplyDeletebodrum
uşak
kumluca
ankara</a
0EPK
https://saglamproxy.com
ReplyDeletemetin2 proxy
proxy satın al
knight online proxy
mobil proxy satın al
L3E4