Utunzaji bora wa majike ni muhimu kwani utamuwezesha mfugaji
kupata Mawazo mengi na bora.Majike azazi watunzwe vizuri ili kuongeza idadi Ya
watoto watakaozaliwa kwa mwaka na kuongeza faida kwa mfugaji. Utunzaji bora ni
kiini cha idadi ya watoto watakaozaliwa,watakaoishi na Muda wataochukua kufikia
uzito kuuza na gharama zitakazotumika.
Kuchagua jike Bora
Mfugaji anashauriwa kuchagua nguruwe jike anayetegemewa kuwa
mzazi kwa kuzingatia sifa zifuatazo:-
- ·Awe amezaliwa na mama anayezaa watot wengi,menye kutoa maziwa mengi na mtunzaji mzuri wa watoto
- · Awe na afya nzuri
- · Awe na kiwele kikubwa chenye chuchu kati ya 10 hadi 14
- · Awe ni MRE na mwenye uwiano mzuri kati ya urefu, upana na kimo
- · Awe na umbile la kumuwezesha kubeba mimba na kuzaa kwa urahisi
- · Awe na miguu imara iliyonyooka,kwato imara,mgongo wenye nguvu na uliopinda kiasi
- · Awe mpole
- · Atokane na wazazi wasiokuwa na historia ya magonjwa au klema cha kurithi.
Taratibu
za kupandisha majike
Nguruwe kike anaanza kuonyesha dalili za
joto akiwana umri wa miezi sitahadi saba.Hata hivyo, inasshauriwa kutompandisha
kipindi hicho ili kuzuia kuzaliwa watoto wenye uzito mdogo,kupata mtatizo
wakati wa kuzaa,afya mbaya na kudumaa. Hivyo, inapendekezwa nguruwe apandishwe
atakapoonyesha dalili za joto kwa mara ya pili au ya tatu.
Kwa kawaida nguruwe
huwa tayari kupandishwaakiwa na umri wa miezi
kati ya nane na tisa kutegemea afya na aina ya nguruwe.
Kumtambua
Nguruwe Aliye Kwenye Joto
Mfugaji anashauriwa kuwachunguza nguruwe
siochini ya mara mbili kwa siku hususani asubuhi na jioni wakati wa kuwalisha
ili kutambua dalili za joto.
Zifuatazo
ni daliliza nguruwe jike aliye kwenye joto
- · Hupoteza hamu ya kula
- · Hutoa sauti ya kugugumia
- · Huhangaika mara kwa mara
- · Hupandwa na wenzake na hutulia akipandwa au akigandamizwa mgongoni
- · Sehemu ya uke huvimba na huwa nyekundu
- · Hukojoa mara kwa mara na hutoa ute
- · Husimama wima na hutulia akiwa ametanua miguu ya nyuma na mkia ukielekea juu wakati akipandwa na dume.
Dalili hizi sio lazima zionekane zote wakati mmoja hivyo ni
jambo la muhimu kuwa mwangalifu.Ili dalili hizi ziweze kuonekana vizuri,chumba
cha majike yanayotarajiwa kupandwakinatakiwa kiwe karibu na cha dume.
Joto hudumu kwamuda wa sikumbili hadi tatu.Nguruwe jike
apandishwe mara mbili kwa siku hususani asubuhi na jioni.Nguruwe apandishwe
masaa 12 hadi 24 anapoonyesha dalili za kusimama akipandwa na dume au
akigandamizwa mgongoni.Kwa kawaida nguruwe hurudia kuingia kwenye joto kila
baada ya siku 21 ikiwa hana mimba.Mfugaji anashsuriwa kumchunguza ngurwe jike
baada ya kumpandisha aingia kwenye joto baada ya kupandishwa.
Wakati wa kupandisha inashauriwa nguruwe jike kupelekwa
kwenye chumba cha dume ili kuzuia dume kushambuliwa na jike.Nguruwe ambaye
hashiki mimba baada ya kupandishwamara nyingi inashauriwa mfugaji kumuona
Daktari wa mifugo kwa ushauri.
Ulishaji wa jike
Kabla ya kupandishwa nguruwe jike apewe kilo 2.5 hadi 3 za
chakula kwa siku na kupewa maji safi na ya kutosha wakati wote.
Kutunza Nguruwe Wenye
Mimba
Utunzaji bora wa nguruwe wenye
mimba ni muhimu katika kupata watoto wenye uzito mkubwa na afya bora.Pia
husaidia nguruwe kuwa na afya bora,kutoa maziwa mengi nakupunguza vifo vya
watoto.
Mimba ya nguruwe huchukua siku
114hadi 119(miezi mitatu,wiki tatu na siku tatu) hadi kuzaa.Kwa kipindi hicho nguruwe
anahitaj lishe bora na maji,hewa safi nay a kutosha, mazoezi pamoja na kinga
dhidi ya magonjwa.Hivyo, inashauriwa banda liwe na nafasi ya kutosha, na safi
muda wote.
Ulishaji wa Nguruwe Wenye Mimba
Nguruwe mwenye mimba anahitaji kupewa cha kula kinacholeta nguvu na kujenga mwili. Inashauriwa, mwezi wa kwanza wa umri wa mimba apewe kilo 2 hadi 2.5 kwa nguruwe mwenye afya nzuri, akiwa dhaifu apewe kilo 3 kwa majuma matatu. Pia, baada ya siku 84 za umri wa mimba apewe kilo 2 za chakula kwa siku na kuongeza nusu klo kila wiki mpaka siku ya tatu kabla ya kuzaa. Siku tatu kabla ya kuzaa, chakula kipunguzwe hadi kufikia kilo 2 kwa siku na wapewe majani kama luseni au chakula chenye nyuzi nyuzi nyingi kama pumba kilo moja kwa siku tatu kabla ya kuzaa ili kuzuia tatizo la kinyesi kuwa kigumu ambacho hushindwa kutoka na kusababisha nguruwe kuzaa kwa shida. Siku ya kuzaa nguruwe asipewe chakula apewe maji tuu.
kinga dhidi ya Maginjwa na Wadudu
Nguruwe wenye mimba huathiriwa zaidi na minyoo na magonjwa mengine. Minyoo hupunguza hamu ya kula na hivyo huathiri afya ya nguruwe pamoja na ukuaji wa mimba. Uzuiaji wa magonjwa na wadudu ni muhumu kwa afya ya nguruwe mwenye mimba. Mfugaji anashauriwa kuwapa nguruwe dawa ya kuzuia minyoo siku 21 hadi 28 kabla ya kuzaa.
Kuzuia wadudu, mfugaji anashauriwa kuogesha kwa dawa zakuogeshea angalau mara mbili kwa wiki ili kuzuia ukurutu na matatizo mengine ya ngozi. kwenye sehemu ambazo kuna ndorobo, mfugaji anashauriwa kuwachanja nguruwe. Ni muhimu banda na vifaa vya kulishia na maji viwe safi wakati wote.
ITAENDELEA MAKALA HII NZURI KUHUSU UFUGAJI WA NGURUWE AMBAPO TUTAANGALIA MAANDALIZI KABLA YA NGURUWE KUZAA
Naitwa Bruno naomba kujua ngurue aliezaa na akatoa maziwa kwa siku 4 na kushindwa kuendelea kunyonyesha je tatizo nini na Tiba take
ReplyDeletempe chakula cha kutosha chenye madini na protini kwa wingi...na maji ya kutosha
DeleteSafi
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu
ReplyDeleteAsante sana kwa somo zuri
ReplyDeleteAhsante kwa elimu nzuri! Samahani hivi nguruwe anatakiwa kula mara ngapi Kwa siku wastani
ReplyDeleteSomo ni zuri
ReplyDeleteSikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
ReplyDelete* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
* kuvunja obsessions
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* uchawi wa bahati
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159
Samhani mim nguluwe wangu Amepata joto ni kwa mala ya kwanza na imepandwa je kunaweza kua na tatzo juu ya hapo
ReplyDeleteNachoomba kujua kama kuna tatz ngulew wangu toka wadogo mbaka wanakua nina walisha pumba za mpunga zipe laini jr kuna naam ya kosa hapo au inaitajika mixa yoyote
ReplyDeleteasante kwasomo zuri lakn pia nguruwee endapo anaujauzto anatakiwa apewe dawa yaaina gani maana zpo nyng
ReplyDeleteNguruwe baada ya kuzaa anaingia kwenye joto tena baada ya siku ngap? Au muda gan?
ReplyDeleteMatuzo yapi ni Bora kwa nguruwe jike kwa ajil ya kuzalisha mayai mengi wa kati wa kupandishwa
ReplyDelete