Mbegu ndio msingi wa kiumbe hai chochote. Mbegu za mazao kama mpunga hutunza sifa za kijenetiki za mmea hivyo matumizi ya pembejeo zingine za kilimo ni katika tu kusaidia mbegu iweze kutoa mavuno kwa kiwango kinachotegemewa. Ndio maana pembejeo zingine kama mbolea zisipotumika mbegu huweza kutoa mavuno kidogo tu lakini pembejeo zingine hizi haziwezi kutumika bila mbegu.
1. Umuhimu na
kanuni za mbegu bora.
a. Kwanini mbegu
bora?
Mbegu bora za mpunga
zimetafitiwa ili kukidhi mahitaji ya wadau muhimu katika sekta ya
mpunga kama vile:
i. Wakulima --- Mavuno mengi
ii. Wasindikaji --- Ukobolekaji
iii. Wafanyabiashara --- Mwonekano k.m. punje ndefu na
nyembamba
iv. Walaji --- Radha, kupikika,
b. Faida za
kutumia mbegu bora
- Zimetiwa
dawa ya kuzuia magojwa ya udongoni, vijidudu na fangasi hivyo
kuiepusha mbegu na mche kutokana na mashambulio ya magonjwa, wadudu
na fangasi.
- Zina uotaji
wa kiwango cha juu hivyo huokoa gharama ya mbegu. TOSCI hudhibitisha
mbegu ya mpunga ikiwa tu uotaji wake ni zaidi ya 80%.
- Huokoa
gharama
Mfano:
Jedwali la matumizi ya mbegu katika
Ekari moja na gharama zake
Mbegu
|
Kiasi cha mbegu kwa Ekari
|
Gharama ya mbegu
|
Jumla ya gharama ya mbegu
|
Mbegu bora iliyothibitishwa
|
Kilo 4 hadi 8
|
TSH 3,000 kwa kilo
|
12,000 hadi 24,000
|
Mbegu isiyo bora
|
Debe 2 hadi 3
|
TSH 10,000 kwa debe
|
20,000 hadi 30,000
|
c.
Mbegu bora
- Ni halisi (genetic pure)
- Ni safi, haina mchanga, mapepe wala masuke
- Viwango vya uotaji viko juu
- Hutoa mimea yenye afya njema
- Huvumilia baadhi ya magonjwa na wadudu
- Hukomaa pamoja
- Mchele wake huiva kwa pamoja ukipikwa
- Ni safi, haina mchanga, mapepe wala masuke
- Viwango vya uotaji viko juu
- Hutoa mimea yenye afya njema
- Huvumilia baadhi ya magonjwa na wadudu
- Hukomaa pamoja
- Mchele wake huiva kwa pamoja ukipikwa
2. Uzalishaji
wa mbegu bora
a.
Uchaguzi wa shamba na maandalizi kwa ajili ya
uzalishaji wa mbegu
Sifa za shamba
i. Tambarare, lisilo na miinuko
ii. Lisilo na mafuriko
iii. Lisilo na vivuli
iv. Kuingiza maji na kuyatoa kiurahisi (good drainage)
ii. Lisilo na mafuriko
iii. Lisilo na vivuli
iv. Kuingiza maji na kuyatoa kiurahisi (good drainage)
b.
Kukokotoa Kiasi cha mbegu
Kiasi cha mbegu = mbegu
inayotakiwa kwa ekari x eneo (ekari)
Uotaji
(%)
c.
Utenganisho wa shamba la mbegu ya na mashamba
mengine ya mpunga
Uchavushaji waweza kusababishwa
na:
- Upepo
- Wadudu
- Ndege
- Konokono
- Maji
- Wadudu
- Ndege
- Konokono
- Maji
Shamba la mbegu ya mpunga
iliyothibitishwa litengane na mengine kwa mita 5
d.
Uthibiti magugu
Magugu hupunguza wingi na ubora wa mbegu
Shamba liwe safi muda wote
Sheria mbegu imekataza aina fulani ya magugu kutokuwepo kabisa shambani k.m bhangi, mpunga pori, kiduha
Shamba liwe safi muda wote
Sheria mbegu imekataza aina fulani ya magugu kutokuwepo kabisa shambani k.m bhangi, mpunga pori, kiduha
e.
Kuondoa mimea isoyo mbegu (off-type)
Mfano wa off-type
- Mimea ya mpunga iliyojiotea
yenyewe mathalan kutoka msimu uliopita
- Kubadilika kwa sifa za kijenetiki za mmea
- Mchanganyiko wa mbegu kwa bahati mbaya
- Kubadilika kwa sifa za kijenetiki za mmea
- Mchanganyiko wa mbegu kwa bahati mbaya
Utambuzi wa off-type
- Mimea mifupi ama mirefu zaidi ya
wenzao shambani
- Mimea yenye rangi tofauti za majani, masuke
- Mkia wa punje (awn)
- Mimea inayowahi zaidi ama kuchelewa zaidi kuchanua (mimea itofautiane kati ya siku 2-3)
- Mkao wa jani la juu katika suke (lag leaf angle)
- Ukubwa, umbo na rangi ya punje
- Mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa/wadudu
- Mimea yenye rangi tofauti za majani, masuke
- Mkia wa punje (awn)
- Mimea inayowahi zaidi ama kuchelewa zaidi kuchanua (mimea itofautiane kati ya siku 2-3)
- Mkao wa jani la juu katika suke (lag leaf angle)
- Ukubwa, umbo na rangi ya punje
- Mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa/wadudu
Kuondoa maotea (off-type)
kufanyike angalau mara moja wakati wa:
- hatua ya ukuaji wa majani
(vegetative growth)
- kuchanua
- baada ya kuchanua
- kabla ya kuvuna
- kuchanua
- baada ya kuchanua
- kabla ya kuvuna
f.
Udhibiti wa wadudu na magonjwa shambani
Ifahamike kwamba, wadudu na magonjwa huathiri wingi na ubora wa mbegu ya mpunga hasa viwapo shambani.
Ifahamike kwamba, wadudu na magonjwa huathiri wingi na ubora wa mbegu ya mpunga hasa viwapo shambani.
g.
Matumizi ya mbolea
Matumizi sahihi ya mbolea huongeza ubora na wingi wa mavuno ya mbegu ya mpunga.
Matumizi sahihi ya mbolea huongeza ubora na wingi wa mavuno ya mbegu ya mpunga.
3. Uvunaji
na huduma baada ya kuvuna mbegu bora
a.
Muda wa kuvuna (Timing)
Kuwahi ama kuchelewa hupunguza ubora na mavuno
Athari ya Kuwahi kuvuna
-
Mbegu zisizojaza vizuri
- Mavuno/ubora kidogo
- Kupoteza uotaji
- Mavuno/ubora kidogo
- Kupoteza uotaji
Athari za Kuchelewa kuvuna
- Mashambulizi ya wadudu, ndege
- Kuanguka
- Kupukutika
- Mashambulizi ya wadudu, ndege
- Kuanguka
- Kupukutika
Muda
sahihi wa kuvuna
-
Punje hugeuka kuwa njano-kahawia
- 80% ya majani imebadili rangi kutoka kijani na kuwa rangi ya mabua
- Unyevu wa punje 20-22%
- Punje huwa ngumu na hazivunjiki kirahisi zikitafunwa
- 80% ya majani imebadili rangi kutoka kijani na kuwa rangi ya mabua
- Unyevu wa punje 20-22%
- Punje huwa ngumu na hazivunjiki kirahisi zikitafunwa
b.
Kukausha mbegu ya mpunga
Mbegu yenye unyevu kidogo huweza
kutunzwa kwa kipindi kirefu bila kuharibika (kuvuna, kupoteza uotaji).
Unyevu wa mbegu
|
Muda wa kudumu gharani
|
14-18%
|
Wiki 2 -3 tu
|
13%
|
Miezi 8-12
|
9%
|
Zaidi ya mwaka
|
4.
Viwango vya mbegu
Mbegu
bora huzalishwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu hivyo vimewekwa viwango ambavyo
ili mbegu ithibithishwe ni lazima vifikiwe.
Vipo
viwango vya shambani na maabara kama ifuatavyo:
a. Viwango vya shambani
Kigezo
|
Kiwango
|
Shamba
(misimu kabla)
|
2
|
Utenganisho
|
mita
5 na zaidi
|
Awamu
za ukaguzi
|
2
na zaidi
|
Maotea
(off-types)
|
0.1
|
Mazao
mengine
|
0.05%
|
Magugu
yaliyozuiwa
|
0
|
Mimea
ya Mpunga pori
|
0.1%
|
b. Viwango vya maabara
Kigezo
|
Kiwango
|
Mbegu halisi (Pure Seed)
|
98.0% na zaidi
|
Mbegu zingine (Other Seed)
|
0.1
na pungufu
|
Makapi (masuke, vijiti, majani)
|
1.9% na pungufu
|
Unyevu wa mbegu
|
13.0% na pungufu
|
Uotaji
|
80% na zaidi
|
Mbegu za magugu yaliyozuiliwa
|
0.0%
|
Mbegu za magugu yayokatazwa
|
punje 4 kwa kilo na pungufu
|
Baadhi
ya Magugu yaliyozuiliwa
-
Kiduha/Magugu
chawi (sani)
-
Bangi
-
Kokeini
Magugu
yaliyokatazwa
-
Ndago
-
Mpungapori
-
Mashikanguo
Imeandaliwa na: Happy Sikalengo 0755325442
0 comments:
Post a Comment