Kutokana na kupanda kwa gharama za matumizi ya umeme na athari zinazotokana na umeme watu wengi wamegeukia chanzo mbadala cha energy(power). Moja ya chanzo mbadala cha umeme siku hizi ni nishati itokanayo na jua hapa chini ni historia fupi ya umeme utokanao na jua yaani solar power system.
HISTORIA YA UMEME WA JUA (SOLAR SYTEM)
Historia ya umeme wa nishati ya jua ulianza mnamo mwaka 1876 Willium Grylls Adams na mwanafunzi wake Richard day walipogundua kuwa selenium ikiwekwa kwenye jua itazalisha umeme. Baada ya hapo mtafiti mwingine aitwae Werner von Siemens akaja na idea kuwa selenium sio nzuri sana na kusema kuwa unaweza zalisha umeme bila heats (joto) na vitu vinavyotembea (moving parts).
1953, Calvin Fuller, Gerald Pearson, and Daryl Chapin waligundua seli ya siliconi. Na kuhakikisha ndio seli ambayo inaweza kuzalisha umeme wa kutosha na hapo ndipo gazeti la new york times lilipochapisha "the beginning of a new era, leading eventually to the realization of harnessing the almost limitless energy of the sun for the uses of civilization."
Mwaka 1956 seli ya silicon ilikuwa ikipatikana sokoni rasmi kwa ajili ya matumizi ya solar power. Na mnamo mwaka 1960 satellite nyingi za USA's na Soviet,s zikaanza kuendeshwa kwa kutumia solar seli.
Mwaka 1970 hadi 1990 solar seli zilianza kutumia kwenye taa za kuongozea magri yaani (traffic light), matumizi vijijini ambako grid ya taifa ilikuwa haijafika, kupower vifaa vidogo vya electroniki kama saa,kikokotozi.
Hadi sasa nishati ya jua imekuwa kwa kiwango kikubwa na imepunguza kwa kiwango kikubwa uharibifu wa mazingira hasa kwa watu wanaishi vijijini mfano watu walikuwa wakitumia taa za mauta ya taa lakini sasa wanatumia taa ndogo za kuchagi na mwanga wa jua. Kwa hapa tanzania hii ni nishati iliyoleta mabadiliko makubwa sana hasa vijijini na imepunguza kwa kiwango kikubwa gharama za maisha kutokana na matatizo ya kukatika katika kwa umeme hasa kipindi cha kiangazi.
MAANA YA NISHATI YA JUA (SOLAR POWER SYSTEM)
Huu ni mfumo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua kupitia solar seli ambapo miale ya mwanga hutua moja kwa moja au kwa kutumia lenzi ili kukusanya miale mingi na kuielekezea kwenye seli hizo kwa lengo la kupata kiwango kikubwa cha umeme . Pindi tu miale ya mwanga inapotua kwenye seli eletroni zinaondolewa kutoka kwenye atom yake na kupelekwa kwenye high energy level na kusababisha movement ya electroni kwa kuwa kunakuwa na metal mbili zilizowekwa moja juu ingine chini ya solar seli inazichkua hizo seli na kufanya umeme. Hii inafanyika kwa sababu matilio ilyotumika ni semikonducta. Hapo ndipo umeme unapozalishwa.
USIKOSE KUFATILIA MWENDELEZO WA MAKAL HII NZURI KWA LENGO LA KUKUZA TEKNOLOGIA YA UMEME VIJIJINI TOA MAONI YAKO HAPO CHINI AU MASWALI YOYOTE KUHUSIANA NA MADA HAPO JUU YATAJIBIWA
MAKALA ILIYOPITA
Naitaji soral number 0684405854
ReplyDelete