Thursday, August 4, 2016

AINA ZA PANELI ZA SOLAR POWER SYSTEM


Baada ya kuangalia aina tatu za solar power syatem katika makala ilipopita, Leo tunaenda kuangalia aina za paneli za solar na matumizi yake katika kuzalisha nishati ya umeme . Zifuatazo ni aina mbalimbali za solar panel zinazopatikana sku hizi duniani kwa ujumla na tutaona ipi inafaa kulingana na uchumi wa mtanzania wa chini,uwezo wa kukidhi malengo na kadhalika:-



1. Monocrystalline Silicon (Single Silicon)
hadi sasa inasemekana hii ndio aina ya panel yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme pale tu ambako nguvu ya jua ikitua kwenye hizo paneli. Kuwa na uwezo mkubwa kunatokana na wingi wa silicon katika panel hiyo yaan silicon content is high compared to other. Pia aina hii ya panel inauzwa ghali sana lakini unaitaji tuu chache tu kwa kuzalisha umeme wa kutosha kutokana na matumizi yako. Kwa hiyo msomaji wa makala hii ukiitaji kununua solar panel hii inafaa sana kutokana na faida zake hapo juu na unahitaj panel chache tu moja inategemea na matumizi yako.

Huu ndio mwonekano wake 

Types of Solar Panels for Residential Solar


2.Polycrystalline Silicon (Multi-silicon)

hii ni aina ya pili ambayo inatofautiana na "mono" kwa kuwa na kiwango kidogo cha silicon ukilinganisha na monocrystalline panel. Kutkana na hivyo hata efficient yake ni ndogo ukilinganisha na aina ya kwanza. Pia inauzwa kwa gharama ndogo ukilinganisha na ya kwanza.Kwa hiyo hii ni aina nzuri kama ukishindwa kuafford kununua aina ya kwanza bila kusahau faida yake kubwa ni nzuri kwa kuezulia paa la nyumba kutokana na ilivyotengenezwa inauwezo wa kucool room yako na nyumba kwa ujumla.

mwonekano wake

Polycrystalline silicon solar panels

3. BIPV (Building Integrated Photovoltaics)

Hii ni aina nyingine ya solar panel ambayo inamwonekano mzuri na pia inatumika kwa roof tiles. Kutokana na hivyo hata gharama yake ni kubwa lakini ina uwezo mdogo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua. Kwa hiyo si panel nzuri sana kwa matumizi hasa mtanzania hata baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji yameacha kutengeneza na ukitaka ni kwa oda maalumu.

muonekano wake

Types of Solar Panels for Home Solar


4. Solar Thermal Panels

Hii ni aina nyingine ya solar panel ambazo hazizalishi umeme bali zinapasha maji joto kwa matumizi ya majumbani na taasisi mbalimbali kama hostels (new hostel sua) ,hospitali na hata kwenye mashule mbalimbali hasa wakati wa baridi. 

Solar Thermal Panel

HIZI NI AINA CHACHE ZA SOLAR PANEL ZINAZOTUMIKA KWA WINGI HASA HAPA TANZANIA.

NDUGU WASOMAJI WA MAKALA HII NAWAKALIBISHA KWA MAONI YENU NA MASWALI NA KUONGEZEA UJUZI MAALI AMBAKO SIJAELEZEA VIZURI AU IDEA MPYA ITAYOJENGA 

KWA WALE WALIOKOSA MAKALA ILIYOPITA BOFYA HAPA
Share:

1 comment:

  1. Kutana na mtaalamu wa mitishamba ..anatibu ugumba..uzazi..nguvu za kiume..kubana uke..hips shape na makalio...mapenz zindiko ..uchawi....kuondoa harufu mbaya na maji ukeni..wasiliana na dr kanyas 0744903557 ofis kuu tanga

    ReplyDelete

Blog Archive

Latest Posts

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support