Friday, August 12, 2016

Panda Mpunga kwa nafasi ili upate mavuno zaidi na uokoe gharama ya mbegu


Panda kwa nafasi zilizopendekezwa na wataalamu. Kumbuka kuwa na idadi ya mimea inayopendekezwa shambani ni chanzo cha mavuno mengi kwani wingi wa mimea unamaanisha wingi wa wazazi shambani.
Panda kwa msitari ili kurahisisha zoezi la palizi, utiaji mbolea na uvunaji.
Nafasi zitumikazo kupanda mpunga shambani.
Nafasi kati ya shina na shina (Sm)
Idadi ya mimea katika Ekari
Idadi ya mimea katika Hekta
20 kwa 20
100,000
 250,000
15 kwa 15
177,778
 444,444
15 kwa 20
133,333
 333,333
25 kwa 25
 64,000
 160,000
25 kwa 20
 80,000
 200,000
Hata hivyo, uchaguzi wa vipimo vya kutumia shambani hutegemea:
a.    Aina ya mbegu, ndefu-mbali mbali, fupi – karibu karibu

b.    Rutuba ya shamba, rutuba nyingi – karibu karibu, rutuba kidogo – mbali mbali
Share:

1 comment:

  1. Kilimo hiki hata mimi natamani sana kukifanya.kwa hiyo naombeni msaada mfano nata nilime ekar moja naweza tumia gharama kiasi gani na kama hutojali unaweza kuionyesha kwa table ili nielewe vema

    ReplyDelete

Blog Archive

Latest Posts

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support