Katika makala iliyopita tuliangalia historia fupi ya solar power system ilivyoanza, wakina nani waligundua pia tuliona maana yake na kuangalia kwa ufupi sana jinsi inavyozalisha umeme.Pia tuliona kuwa nishati hii ya jua yaweza kutatua matatizo yanayomkabili mwananchi wa hali ya chini katika upatikanaji wa nishati hasa vijijini.
Kutokana na utangulizi mfupi hapo juaa leo tunaangalia kuna aina ngapi za solar power system zinazotumika hasa hapa Tanzania:-
1. SOLAR POWER SYSTEM INAYOZALISHA UMEME (PV CELL)
Hii ni aina ya solar inayopatikana hasa hapa nchini kwetu, Inatumia mwanga wa jua kuzalisha umeme unaotumika kwa matumizi mbalimbali kama umeme majumbani, taa za kuongozea magari balabalani, kucharge battery za simu zetu, torch na matumizi mengineyo. Kwenye huu mfumo kinachifanyika ni kupakua photoni zote zinazofikia solar seli na kubadili kwenda kwa electrical currenti ambapo umeme unaozalishwa unakuwa ni direct current kwa ajili ya matumizi mbalimbali kushirikiana na mifumo mingine ambayo tutaiangalia baadae kwa ajili a kubadilisha dc kwenda ac.
2. SOLAR POWER SYSTEM INAYOPASHA MAJI MOTO (SORAL THERMAL)
Hii ni aina nyingine ambayo imepata umaarufu mkubwa sasa hapa tanzania hasa sehemu zenye baridi kama mikoa ya iringa.mbeya,kilimanjaro,arusha na singida na mingine mingi. ambako huu mfumo unatumia nishati ya juu kupasha joto maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Tutaelezea kivipi huu mfmo unafanya kazi hapo baadae kwa hiyo fatilia vizuri huu mwendelezo wa hii makala tushare idea na waweza tengeneza huu mfumo mwenyewe na kukuingizia kipato hasa vijana wanaokumbwa na tatizo la ajira.
3. SOLAR POWER SYSTEM INAYOKAUSHA NAFAKA NA KWA AJILI YA RESEARCH
Hii ni aina nyingine ambayo imekuwa ikitumika kwa kukaushia mazao na samples kwa ajili ya research. ni mfumo mzuri ambako tutaona jinsi ya kuutengeneza na faida zake hapo baadae keep update msomaji wa makala hii nzuri inayoelimisha.
USIKOSE MAKALA INAYOFUATA YA AINA ZA SOLAR PANEL N AJINSI ZINAAVYOTUMIKA SHARE NA RAFIKI AKO ASOME
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI NA MASWALI YOTE
MAKALA ILIPOPITA
0 comments:
Post a Comment