Ndugu zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada
yangu, mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa
Blogu ya WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha
nikamshirikisha harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa,
akaniomba niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi
nikakubaliana na ombi hilo.
Unaweza kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea.
Chunguza marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze
kwao na usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa
samaki, kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea,
usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to
get you anywhere’ GO BIG OR GO HOME.
Ninachokiamini katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi
kubwa sana ya kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo
atajitambua na kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote
anaetambua uthamani wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea
kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.
Ndugu zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada
yangu, mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa
Blogu ya WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha
nikamshirikisha harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa,
akaniomba niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi
nikakubaliana na ombi hilo.
Unaweza kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea.
Chunguza marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze
kwao na usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa
samaki, kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea,
usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to
get you anywhere’ GO BIG OR GO HOME.
Ninachokiamini katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi
kubwa sana ya kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo
atajitambua na kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote
anaetambua uthamani wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea
kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.
Katika Makala yangu ya wiki hii ningependa kuwashirikisha kitu kidogo
sana nacho ni UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI
MDOGO SANA… kipindi cha nyuma, nilikuwa nikiwaona watanzania wenzangu
hasa huku Iringa, wakijishughulisha na ufugaji wa samaki, ni miaka
miwili imepita sasa, lakini nilikuwa ‘bize’ na mambo yangu sikutaka
kujifunza Zaidi kuhusu fursa hii. Mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka
jana 2014 rafiki yangu Nicolaus Kulangwa, ambae huko nyuma alinifundisha
kilimo cha Matango,alinipigia simu akinitaka nikataembelee mradi wake
wa kufuga samaki. Nilienda kijini kalenga hapa Iringa. Nilichokiona
nilianza kukifanyia kazi hapohapo na siku ileile. Wakati rafiki yangu
akiwa na jumla ya mabwawa saba ya samaki aiana ya sato na pelege mimi
ndio kwanza nilijutia muda ambao niliambiwa kuhusu fursa ile halafu
nikazembea kuifanya.
Kama tunavyofahamu, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya
unachokifanya na kugusa jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo
kwa mifugo mingine yeyote ile, kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu
yanayopaswa kuzingatiwa ili ufugaji wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa
na hivyo kufikia malengo ya mfugaji huyo. Lakini kutokana na mazingira
ya ufugaji wa huku Iringa hasa Kalenga, nitayataja mambo hayo kwa kifupi
sana, mambo haya huenda yakatofautiana kutoka eneo moja la nchi hadi
jingine, na kwa vile mimi sijasomea chuo cha ufugaji wa samaki, maelezo
haya ni yale niliyoyapata kwa uzoefu tu, siyo ya kufundishwa chuo,
mapungufu yatakayogundulika na ‘wasomi’ wataniandikia email ili
nikawashirikishe wenzangu.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo:
ENEO AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI. Inasisitizwa kwamba, eneo
hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu maji kupotea hovyo. Udongo
wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa tifutifu ama
udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti ama kuweka
‘kapeti gumu’ lisilo ruhusu maji kupotea.
UPATIKANAJI WA MAJI, wote tunafahamu kwamba samaki huiishi
majini, maji ndiyo roho ya masaki, samaki ni maji na maji ni samaki.
Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na maji ya kutoshana salama kwa
kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji kwa ajili ya ufugaji wa samaki
ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji ya ardhini hasa visima Kwa
maeneo ya huku Iringa, tunabahati ya kuwa na mto Ruaha ambao maji yake
yapo muda wote wa kipindi chote cha mwaka. Inashauriwa kwamba eneo hilo
liwe salama ili kuwalinda samaki na mfugaji kwa ujumla.
BWAWA. Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye
mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya
ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi
linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
MBEGU AMA VIFARANGA, mfugaji wa samaki anashauriwa kutembelea
maeneo ambayo wafugaji wakubwa wanazalisha vifaranga ili aweze kupata
mbegu bora anayohitaji. Kwa wananaoishi Iringa na maeneo ya jirani,
wanaweza kupata mbegu kwa bwana Nicolaus.
UTUNZAJI WA BWAWA NA USAFI. Ili mfugaji aweze kunufaika na miradi
ya kufuga samaki ni lazima uafanye usafi wa kutosha ndani nan je ya
bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu na viumbe
wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge wasiweze kufanya makazi na
hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara
moja.
ULISHAJI. Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji
kula chakula kingi sana. Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza
kuwa mara tatu kwa wiki ama Zaidi.
AINA YA CHAKULA. Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya
mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga
zilizosagwa, unga wa mahindi, mabaki ya chakula kama ugali nk.
Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo
mengine ni kama vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia
masoko, utaalamu nk.
CHANGAMOTO KATIKA SAMAKI ni magonjwa kama vile magonjwa ya samaki
yapo mengi yakiwa nayasababishwa na vimelea vifuatavyo magonjwa
yanayosababishwa na bakteria, magonjwa yanayosababishwa na virusi
magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa yanayosababishwa na
protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni. Chanagamoto nyingine
ni kama vile, Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo
hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za
ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Iwapo
bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi
bwawani kupita idadi inayotakiwa.
UVUNAJI WA SAMAKI. Hujudi za mfugaji ndio zinaweza kupelekea
kuvuna samaki wa kutosha na kumletea faida kwa muda mfupi. Wakati wa
kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji
wa samaki pia hutegemea ubora wa chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa
lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8. Kuna
watakao sema huu ni muda mrefu, ukiona ufugaji wa samaki wanatumia muda
jaribu kingine. Ama endelea kukaa nyumbani kwako, ukiisubiri serikali na
mashirika ya kijamii yakusaidie.
Nielezee kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi
kwa watanzania na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za
kiuchumi, na ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa,
imesababisha watanzania wengi kuanza kuwa wabunifu na kuanza
kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji. Kwa sasa mabwawa
mengi yanapatikana katika mikoa sita yenye rasilimali nyingi kama
Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma. Ufugaji wa
samaki umeenea kote nchini.
Kwa sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/ kwa huku Iringa na
ukiuuzia bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/ kwa kilo. Hii ina maana
kwamba ukiwa na kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni
mbili na laki nane kila baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa
bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya
sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu tano? Utagundua kwamba adui wa
mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo weka kichwani kwako.
Niseme wazi tu kwamba, ufugaji wa samaki, ni fursa nyingine ambayo ipo
wazi kwa kila Mtanzania kuifanya, kuna watakao singizia mitaji, hali ya
hewa nk,lakini ukweli ni kwamba bwawalangu dogo nilitumia pesa ndogo
sana kulichimba ikiwa ni pamoja kununua vifaranga vya samaki.
Tumekuwa watu wa kujiwekea mipaka ya mafanikio vichwani mwetu. Kumbuka
kwamba ukishajiwekea mipaka ya mafaniko. Maisha yetu yataweza kubadilika
iwapo tutabadilisha namna tunavyoyatazama mambo. Kwa mfano unaweza kuwa
umejiwekea mipaka ya kimapato kwamba wewe mwisho wako ni kupata laki
moja, mtazamo huo ukikaa kichwani basi ukiambiwa bwawa moja linaweza
kukutolea shilingi milioni 25 kwa miezi sita, utakataa na hivyo fursa
hiyo itakupita.
Nilipokuwa nikisoma kitabu cha ‘THE TRUTH SHALL MAKE YOU RICH’ cha
reallionaire mdogo kuliko wote Farrah Gray kwa sasa, nimejifunza kwamba,
maisha yetu yanaweza kubadilika muda wowote na dakika yoyote iwapo
tutajijengea Imani kwamba, maisha yanawezekana popote. Na kwa Tanzania
hii ambapo kila mwananchi anaruhusiwa kulimiliki ardhi kwenye mkoa
wowote umasikini litakuwa ni swala la kujitakia.
Ninamalizia makala hii kwa kusema kwamba, kila saa katika maisha yetu ni
fursa, makala hii pia ni fursa kwako na kwangu, kuna baadhi ya nchi
duniani ambapo wananchi wake hawana bahati ya kukaa kwenye meza zao na
kujifunza mambo haya. Kwawatakao penda kuja Iringa, kujifunza ufugaji wa
samaki, tunawakaribisha sana. Nicolaus na mimi na wafugaji wengine
watakusaidia kuapata elimu Zaidi yahii niliyoandika hapa.
Thursday, August 11, 2016
Home »
ufugaji wa samaki
» FAHAMU JINSI YA KUFUGS SAMAKI KWA MTAJI MDOGO
uko sawa kiongozi
ReplyDelete