Wakulima
wamekuwa wakitumia kemikali kiasi cha kutisha kwenye mazao kwa ajili ya
kudhibiti wadudu.
Kwa mfano uzalishaji wa nyanya unaweza kuwa na
faida kwa mkulima. Msimu ambao nyanya zinakuwa chache bei hupanda mkulima
anapata faida zaidi. Kwa upande mwingine zao la nyanya ni rahisi sana
kushambuliwa na wadudu na magonjwa.
Tatizo moja kubwa la kutumia dawa za kudhibiti
wadudu na magonjwa kwa kiasi kikubwa ni
kuwa wadudu hao huwa sugu baada ya muda mfupi. Wakulima kwa uoga wamebuni njia yao
wenyewe ya kudhibiti wadudu na magonjwa. Imetushangaza na kutushtua kugundua
kuwa baadhi ya wakulima hapa nchini wanatumia dawa ya kuulia kupe kwa ajili ya
kuua wadudu wa nyanya kama vile inzi weupe, vithiripi, utitiri na buibui.
Dawa hii inaruhusiwa kutumika kwa ajili ya
kuogeshea wanyama tu lakini si kwenye mboga ambazo zinauzwa kwa walaji.
Sokoni kuna aina nyingine za dawa ambazo ni hatari
na zilishapigwa marufuku na serikali, lakini cha kushangaza baadhi ya maduka ya
pembejeo bado yanaziuza na wakulima wanatumia.
Aina hizi za kemikali ni hatari sana kwa afya ya binadamu
hasa zinapojikusanya kwa kiasi kikubwa mwilini. Baada ya muda mrefu inaweza
kuwa sugu na kusababisha magonjwa ambayo pia ni sugu ambayo hata sasa yamekuwa tatizo
kubwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini, kwa mfano saratani, ukuaji usiokuwa
wa kawaida kisukari na magonjwa ya mzio.
Mbali na madhara kwa afya ya binadamu, pia sumu
hizo hupenya na kwenda kwenye maji yaliyomo ardhini na kuyachafua. Sumu hizo huathiri
na kuuwa wadudu muhimu waliomo ardhini ambao huboresha udongo, kuuwa wadudu
muhimu ambao hufanya ushavushaji kwenye mazao, na wadudu wengineo ambao hudhibiti
wadudu waharibifu kwenye mazao na mazingira yetu.
Njia
endelevu za kudhibiti wadudu
Kuna mbinu za kudhibiti wadudu ambazo ni salama kwa
mazingira yetu. Njia hizo zinajumuisha matumizi ya wadudu rafiki kama vile
nyigu, bungo na wengineo kwa ajili ya kudhibiti wadudu hawa.
Endapo
wakulima wataacha kutumia kemikali hizi, wadudu hawa wataweza kudhibiti wadudu
hao waharibifu kwa asili. Endapo madhara makubwa mkulima anaweza kutumia dawa
za asili katika kudhibiti wadudu hawa, dawa ambazo hazina madhara yoyote.
Tumia
dawa za asili
Mojawapo
ya wadudu ambao huwa wakulima hupata shida kuwadhibiti, ni inzi weupe, vithiripi,
buibui wekundu, na vidukari. Wadudu hawa huharibu kati ya asilimia 20-30 ya mazao
na kuendelea. Wadudu kama vithiripi na inzi weupe ni vigumu sana kuwadhibiti
kwa kuwa huzaliana kwenye mazao yanayokua. Hivyo tumia njia ya kujihami kabla.
Badala
ya wakulima kutumia kemikali, wanaweza
kutumia dawa za asili ambazo haziui wadudu rafiki na ambazo pia husaidia mimea
kujijengea kinga dhidi ya magonjwa.
Kuandaa
dawa za asili:
Mkulima anaweza kutumia aina nyingi za mimea katika kutayarisha dawa za asili. Mfano wa mimea hiyo ni pamoja na bangi mwitu,
tangawizi, mlonge, Mwarobaini na pareto. Katakata mimea yote hiyo kwenye debe na uloweke kwenye pipa
lenye ujazo wa lita 200.
Jaza
maji kwenye pipa hilo na uchanganye kwa nguvu sana. Funika pipa hilo vizuri
uhakikishe hakuna hewa inayopita. Ongeza lita moja ya EM na lita 4 za molasesi.
Vundika kwa muda wa siku 7-10. Weka mchanganyiko wa mimea ya dawa kwenye bomba
la lita 20 lililojazwa maji. Nyunyiza kwenye mazao yako angalau mara tatu kwa
wiki. Dawa za asili zinaweza kukinga mazao yako dhidi ya wadudu wote na hata magonjwa,
pamoja na kupata mazao ambayo ni salama kwa afya.
PlayAmo Casinos and Slot Machines - JTM Hub
ReplyDeletePlayAmo Casino Games - The largest 정읍 출장안마 collection 광양 출장샵 of online slots and live dealer 진주 출장안마 casino games from the 경산 출장마사지 best 보령 출장안마 software providers in the industry.