• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, August 25, 2016

FAHAMU KILIMO BORA CHA MDALASINI - CINNAMON


Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa.

AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)

HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu

KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka

UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.

KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini

MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi

JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula

MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.
Share:

FAHAMU KILIMO BORA CHA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka ambayo kwa jina la kisayansi unajulikana kama (Sorghum bicolor), ni mazao yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.
Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.
Mtaama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.
Aina za mtama
Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.
Aina za mtama zinatofautiana kulingana na rangi zake, kuna nyeupe, nyekundu, na kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora.
Serena:  Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Seredo:  Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.
Gadam: Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.
Hakika na Wahi:  Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.
Utayarishaji wa shamba na kupanda
Kwa kawaida mtama hupandwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hupandwa shambani moja kwa moja baada ya shamba kuandaliwa, lakini pia zinaweza kurushwa shambani, kasha zikavurugwa pamoja na udongo. Unapaswa kutayarisha shamba la kupanda mtama, iwe ni kwa ajili ya malisho au chakula kabla mvua za msimu hazijaanza. Zao hili hufanya vizuri zaidi kwenye udongo ulio laini. Linaweza pia kupandwa kwenye udongo ambao haukulimwa vizuri na bado ukaota vizuri.
Nafasi:  Mtama unaopandwa kwa ajili ya malisho, unaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita 75×10. Aina za mtama ambazo zinalengwa kwa ajili ya lishe kwa binadamu na wanyama, zinahitaji nafasi kiasi cha sentimita 60×20. Nafasi hutoa mwanya wa kuwa na kiwango kikubwa cha malisho. Mkulima anaweza kupanda mbegu za mtama kiasi cha kilo 2.4-3.3 kwa hekari moja. Ni mara chache sana mbegu hupandwa kwenye vitalu na kuhamishiwa shambani baadaye.
Kupanda:  Mtama hupandwa mvua zinapoanza kunyesha. Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu kamili wa mvua. Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi inapokuwa na unyevu. Mtama unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa kuandaa shamba.
Mseto:  Unaweza kupanda mtama mseto na mazao jamii ya mikunde, na kuongeza mboji shambani mwako. Hii inaweza kuwa njia nzuri zaidi ya kupata virutubisho vinavyohitajika. Mseto wa mazao jamii ya mikunde inashauriwa iwe ni kama vile maharagwe, kunde, n.k
Uangalizi na utunzaji
Ni lazima kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari kwa mtama unaokusudiwa kwa ajili ya malisho, na nafasi ya sentimita 20 kati ya mstari kwa mtama uliokusudiwa kwa ajili ya chakula na lishe ya mifugo.
Palizi ya mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.
Share:

FAHAMU KILIMO BORA CHA MPUNGA CHA UMWAGILIAJI


Maandalizi sahihi ya shamba ni jambo la msingi katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu bora zinazoshauriwa kutoonyesha matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika uzalishaji. Kimsingi maandalizi ya shamba yanatakiwa yafanyike kwa usahihi
na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa. Zifuatazo ni hatua saba muhimu na za msingi katika kilimo cha mpunga

1. KUSAFISHA SHAMBA
Safisha shamba mapema kabla ya msimu kuanza. Kusanya na kuangamiza visiki na takataka nyingine zote. Masalia ya mazao yanaweza kutumika kutengeneza mbolea  ya mboji. Inapobidi tumia moto kwa uangalifu sana maana moto unaweza kuharibu mazingira, unaua wadudu rafiki, unaharibu udongo na kuteketeza mboji.

2. KULIMA
Kulima husaidia kupunguza kiasi cha magugu, huruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji, hurahisisha mizizi kupenya na kuchanganya masalia ya mazao kwenye ardhi. Wakati wa kulima uangalifu unahitajika ili kuzuia kuharibu usawa wa ardhi. Kina cha kulima kiwe kati ya sentimeta 10 na 15. Ili kurahisisha na kuharakisha kazi ya kulima ni vema kutumia zana/mashine rahisi kama Trekta la mkono na wanyamakazi 

3. KUKARABATI/KUJENGA MAJARUBA
Baada ya kulima hakikisha kuwa kingo za jaruba zimekarabatiwa ili kuweza kuhifadhi maji vema. Kama ni shamba jipya, ujenzi wa kingo za jaruba  ufanyike kwa kufuata utaalamu unaotolewa. Kingo imara ni muhimu kudhibiti vema maji shambani. 
 
4. KUVURUGA
Weka maji shambani kiasi cha sentimeta 3 hadi 5 juu ya usawa wa ardhi ili kukamilisha vema uvurugaji. Jembe la mkono linatumika lakini ili kurahisisha na kuharakisha kazi hii ni vema kutumia trekta la mkono au wanyamakazi. Unapotumia wanyamakazi au trekta la mkono weka maji shambani si zaidi ya siku moja kabla. Shamba lililovurugwa vema huiwezesha mizizi ya miche kupenya vema ardhini.

5. KUSAWAZISHA SHAMBA
Baada ya kuvuruga ni lazima kuhakikisha kwamba shamba limesawazishwa vema. Shamba lililosawazishwa vema linaruhusu usambaaji mzuri  wa maji. Wakati wa kusawazisha kina cha maji kiwe kiasi cha sentimeta 3-5 juu ya usawa wa ardhi Ili kurahisha kazi hii tumia reki ya ubao ili kuvuta udongo kutoka sehemu zilizoinuka kuelekea sehemu zilizo bondeni

6.VYANZO NA ATHARI ZA UPOTEVU WA MAJI YA UMWAGILIAJI
Ili kupata maji ya kutosha inabidi kuhakikisha kwamba upotevu wa maji ya umwagiliaji unapungua kwa kiwango kikubwa na wakulima wanamwagilia maji kwa kiasi kinachohitajika bila kuzidisha kiwango.

Vyanzo vya upotevu wa maji ya umwagiliaji katika skimu za mfano ni pamoja na:
•  Maji yanayopotea kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile midogo ya kusambaza maji mashambani.
•  Maji yanayopotea mashambani wakati wa kumwagilia.

Upotevu wa maji kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile ya kusambaza maji unasababishwa na aina ya udongo uliotengeneza kingo za mfereji, uchafu na matengenezo hafifu ya mifereji.  Katika baadhi ya skimu upotevu wa maji kwenye mfereji mkuu uliosababishwa na kuvuja maji kwenye tuta la mfereji mkuu na kunywea chini ya ardhi ulikuwa mkubwa kiasi cha kuathiri upatikanaji wa maji kwenye  mashamba yaliyoko mbali na banio.Vilevile athari nyingine ilikuwa ni maji mengi kuingia sehemu yasikohitajika na kusababisha tatizo la maji kutuama kwa muda mrefu.Hivyo wakulima wanashauriwa kupunguza upotevu huu wa maji kwenye mfereji kwa kujengea na kusakafia. Upotevu wa maji mashambani wakati wa kumwagilia unasababishwa na kuvuja kwenye tuta linalozunguka jaruba, kunywea chini na kuzidisha kiwango cha maji ya kumwagilia kinachotakiwa. Hii mara nyingi inasababishwa na utengenezaji mbovu wa jaruba. utengenezaji wa majaruba na uimarishaji wa kingo za jaruba umesaidia kupunguza upotevu wa maji kwa kiwango kikubwa na hatimaye kuongeza mavuno na kipato cha mkulima. 

7. UPANDIKIZAJI MPUNGA
Ili kupata mavuno mengi na kukifanya kilimo cha mpunga kuwa cha faida ni muhimu  wakulima kuzingatia mbinu hii muhimu na kuachana na kilimo cha kiholela kwa kumwaga mbegu moja kwa moja shambani. Aidha kwa wakulima wanaofuata kanuni hii wamepata mafanikio makubwa. 

Faida zinazopatikana kwa kupandikiza mpunga
•  Mkulima huweza kuchagua miche bora na mizuri ikiwa  kitaluni.

•  Miche hukua haraka na yenye afya .
•  Kiasi kidogo cha mbegu huhitajika.
•  Mavuno huwa mengi.
Njia  za kupandikiza miche ya mpunga
Zipo njia kuu mbili za kupandikiza miche ya mpunga, nazo ni: 
•  Kupandikiza kwa mistari
•  Kupandikiza bila ya kufuata mistari (Mchaka mchaka).
Aidha kati ya njia hizi mbili, njia ya kupanda kwa mistari ndiyo inayopendekezwa.zaidi. Pamoja na kwamba upandikizaji wa mistari unahitaji nguvu kazi zaidi, njia hii imeonyesha kuwa na mafaniko mengi ikilinganishwa na kupandikiza kiholela. Shamba lililopandwa kwa mistari ni rahisi kupalilia kwa kutumia kipalizi cha  kusukuma kwa mkono. Pia ni rahisi kwa mkulima  kupanga idadi ya mashina/mimea kwa eneo kwa  uchagua nafasi aitakayo itakayompa mazao mengi.

Uandaaji wa miche
Kabla ya kupandikiza miche shambani ni muhimu kufanya maandalizi yafuatayo:  
•  Inashauriwa kumwagilia miche kwanza ili kupata urahisi wa kungo’a
•  Ili kuzuia miche isikatike ovyo, miche ing’olewe kwa kushikwa chini zaidi ya shina
•  Epuka kung’oa miche mingi kwa wakati mmoja
•  Miche ifungwe kwenye mafungu madogo madogo ili kurahisisha usafirishaji na upandikizaji  shambani
•  Miche bora tu ndio ichaguliwe. Sifa za miche bora
•  Iwe na kimo kinacholingana, 
•  Iwe na majani mafupi yaliyosimama, yenye mizizi mingi na yenye afya, isiyoshambuliwa na wadudu wala magonjwa, 
Jinsi ya kupandikiza miche
•  Miche ishikwe  kwa vidole vitatu kama inavyoosha kweye picha chini 
•  Pandikiza kati ya miche 2 -3 kwa kila shina
•  Kwa mafanikio zaidi, miche ipandikizwe katika kina cha sentimita 2-3.
Share:

Friday, August 12, 2016

FAHAMU JINSI YA KUZALISHA MBEGU YA MPUNGA




Utangulizi
 
Picha imechukuliwa kutoka ITV

 



















Mbegu ndio msingi wa kiumbe hai chochote. Mbegu za mazao kama mpunga hutunza sifa za kijenetiki za mmea hivyo matumizi ya pembejeo zingine za kilimo ni katika tu kusaidia mbegu iweze kutoa mavuno kwa kiwango kinachotegemewa. Ndio maana pembejeo zingine kama mbolea zisipotumika mbegu huweza kutoa mavuno kidogo tu lakini pembejeo zingine hizi haziwezi kutumika bila mbegu.

1. Umuhimu na kanuni za mbegu bora.

a. Kwanini mbegu bora?
Mbegu bora za mpunga zimetafitiwa ili kukidhi mahitaji ya wadau muhimu katika sekta ya mpunga kama vile:

i. Wakulima --- Mavuno mengi
ii. Wasindikaji --- Ukobolekaji
iii. Wafanyabiashara --- Mwonekano k.m. punje ndefu na nyembamba
iv. Walaji --- Radha, kupikika,


b. Faida za kutumia mbegu bora
- Zimetiwa dawa ya kuzuia magojwa ya udongoni, vijidudu na fangasi hivyo kuiepusha mbegu na mche kutokana na mashambulio ya magonjwa, wadudu na fangasi.
- Zina uotaji wa kiwango cha juu hivyo huokoa gharama ya mbegu. TOSCI hudhibitisha mbegu ya mpunga ikiwa tu uotaji wake ni zaidi ya 80%.
- Huokoa gharama

Mfano:
Jedwali la matumizi ya mbegu katika Ekari moja na gharama zake
Mbegu
Kiasi cha mbegu kwa Ekari
Gharama ya mbegu
Jumla ya gharama ya mbegu
Mbegu bora iliyothibitishwa
Kilo 4 hadi 8
TSH 3,000 kwa kilo
12,000 hadi 24,000
Mbegu isiyo bora
Debe 2 hadi 3
TSH 10,000 kwa debe
20,000 hadi 30,000

c.    Mbegu bora
- Ni halisi (genetic pure)
Ni safi, haina mchanga, mapepe wala masuke
- Viwango vya uotaji viko juu
- Hutoa mimea yenye afya njema
- Huvumilia baadhi ya magonjwa na wadudu
- Hukomaa pamoja
- Mchele wake huiva kwa pamoja ukipikwa

2.    Uzalishaji wa mbegu bora
a.    Uchaguzi wa shamba na maandalizi kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu
Sifa za shamba
i.            Tambarare, lisilo na miinuko 
ii.            Lisilo na mafuriko 
iii.           Lisilo na vivuli 
iv.           Kuingiza maji na kuyatoa kiurahisi (good drainage)
b.    Kukokotoa Kiasi cha mbegu
Kiasi cha mbegu = mbegu inayotakiwa kwa ekari x eneo (ekari)
                                                                  Uotaji (%)
c.    Utenganisho wa shamba la mbegu ya na mashamba mengine ya mpunga
Uchavushaji waweza kusababishwa na:
- Upepo 
-  Wadudu
-  Ndege
-  Konokono
Maji
Shamba la mbegu ya mpunga iliyothibitishwa litengane na mengine kwa mita 5
d.    Uthibiti magugu
Magugu hupunguza wingi na  ubora wa mbegu
Shamba liwe safi muda wote
Sheria mbegu imekataza aina fulani ya magugu kutokuwepo kabisa shambani k.m bhangi, mpunga pori, kiduha
e.    Kuondoa mimea isoyo mbegu (off-type)
Mfano wa off-type
-  Mimea ya mpunga iliyojiotea yenyewe mathalan kutoka msimu uliopita 
Kubadilika kwa sifa za kijenetiki za mmea 
Mchanganyiko wa mbegu kwa bahati mbaya
Utambuzi wa off-type
-  Mimea mifupi ama mirefu zaidi ya wenzao shambani 
-  Mimea yenye rangi tofauti za majani, masuke 
-  Mkia wa punje (awn) 
-  Mimea inayowahi zaidi ama kuchelewa zaidi kuchanua (mimea itofautiane kati ya siku 2-3) 
-  Mkao wa jani la juu katika suke (lag leaf angle) 
-  Ukubwa, umbo na rangi ya punje 
-  Mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa/wadudu
Kuondoa maotea (off-type) kufanyike angalau mara moja wakati wa:
-  hatua ya ukuaji wa majani (vegetative growth) 
kuchanua 
baada ya kuchanua 
kabla ya kuvuna
f.     Udhibiti wa wadudu na magonjwa shambani 
Ifahamike kwamba, wadudu na magonjwa huathiri wingi na ubora wa mbegu ya mpunga hasa viwapo shambani.
g.    Matumizi ya mbolea
Matumizi sahihi ya mbolea huongeza ubora na wingi wa mavuno ya mbegu ya mpunga.

3.    Uvunaji na huduma baada ya kuvuna mbegu bora
a.    Muda wa kuvuna (Timing)
Kuwahi ama kuchelewa hupunguza ubora na mavuno
Athari ya Kuwahi kuvuna
-       Mbegu zisizojaza vizuri 
-       Mavuno/ubora kidogo 
-       Kupoteza uotaji
Athari za Kuchelewa kuvuna 
-       Mashambulizi ya wadudu, ndege 
-       Kuanguka 
-       Kupukutika
Muda sahihi wa kuvuna
-       Punje hugeuka kuwa njano-kahawia 
-       80% ya majani imebadili rangi kutoka kijani na kuwa rangi ya mabua 
-       Unyevu wa punje 20-22% 
-       Punje huwa ngumu na hazivunjiki kirahisi zikitafunwa

b.    Kukausha mbegu ya mpunga
Mbegu yenye unyevu kidogo huweza kutunzwa kwa kipindi kirefu bila kuharibika (kuvuna, kupoteza uotaji).
Unyevu wa mbegu
Muda wa kudumu gharani
14-18%
Wiki 2 -3 tu
13%
Miezi 8-12
9%
Zaidi ya mwaka


4.    Viwango vya mbegu
Mbegu bora huzalishwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu hivyo vimewekwa viwango ambavyo ili mbegu ithibithishwe ni lazima vifikiwe.
Vipo viwango vya shambani na maabara kama ifuatavyo:

a.    Viwango vya shambani
Kigezo
Kiwango
Shamba (misimu kabla)
2
Utenganisho
mita 5 na zaidi
Awamu za ukaguzi
2 na zaidi
Maotea (off-types)
0.1
Mazao mengine
0.05%
Magugu yaliyozuiwa
0
Mimea ya Mpunga pori
0.1%

                             
b.    Viwango vya maabara
Kigezo
Kiwango
Mbegu halisi (Pure Seed)
98.0% na zaidi
Mbegu zingine (Other Seed)
0.1 na pungufu
Makapi (masuke, vijiti, majani)
1.9% na pungufu
Unyevu wa mbegu
13.0% na pungufu
Uotaji
80% na zaidi
Mbegu za magugu yaliyozuiliwa
0.0%
Mbegu za magugu yayokatazwa
punje 4 kwa kilo na pungufu


Baadhi ya Magugu yaliyozuiliwa
-       Kiduha/Magugu chawi (sani)
-       Bangi
-       Kokeini

Magugu yaliyokatazwa
-       Ndago
-       Mpungapori
-       Mashikanguo



Imeandaliwa na: Happy Sikalengo 0755325442
Share:

Blog Archive

Latest Posts

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support