Kwa
kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi
zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama
na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa
nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa
na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya
kuhifadhia chakula.
Hiki
ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo
imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa
yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi
makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.
Kutokana
na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga
yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya
nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau
mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.
VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza
kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza
kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo
ni kama vifuatavyo:-
UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo
ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu
mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga,
kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo
ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.
DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA
NYUKI.
Mabanda
hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande
zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.
Kuna
sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya
kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-
1.
Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni
sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya
kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu
kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo
mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani
ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.
Nyuki
wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua
kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio
vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.
Pia
mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi,
hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya
mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.
2.
Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda
haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa
kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa
viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.
3.
Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi
wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama
dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi
wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi
sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za
kila mara.
Pembeni
ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka
na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.
MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga
ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi
ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-
1.
Mzinga wa kibiashara
Huu ni
mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna
asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi
kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.
Mzinga
huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-
a.
Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box
ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo
huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye
utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai
pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.
Pia box
hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa
kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo
mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali
unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.
Kwa
kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu
miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita
mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na
kuendelea.
b.
Kitenga malikia
Hiki ni
kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu
huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga
mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi
peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye
super box.
c.
Box la kuhifadhia asali
Hili ni
box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu
kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa
katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana
na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa
nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa
kuangulia watoto wa nyuki.
Uvinaji
wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box
ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa
kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza
kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.
Mara
baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na
frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki
kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na
hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu
ni kwamba huwezi kupata zao la nta.
2. Mzinga wa viunzi
Huu ni
mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea
mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na
uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu
masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega
moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.
Mzinga
huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya
malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza
kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali
hiyo.
Uvunaji
wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na
kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia
mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.
PICHA ZA MABANDA TOFAUTI TOFAUTI YA KUFUGIA NYUKI
Picha 2:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi
Picha 3:Nyumba ya kufugia nyuki iliyojengwa kwa matofali na kuwekewa
midomo maalumu ya nyuki kwa ajili ya kuingia na kutoka pindi
wanapokwenda kutafuta chakula
Picha 4:Kibanda kidogo cha kisasa kwa jili ya kufugia nyuki.
Picha 5:Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa bati
Picha 6: Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti, kuezekwa kwa bati na kuwekewa uzio wa waya.
0 comments:
Post a Comment