maharagwe machanga yakiwa tayari yamevunwa
Hivi karibuni hapa nchini Tanzania, kumekuwa na uanzishaji na
uendelezaji wa kilimo cha mazao mapya ambayo hayakuzoeleka hapo awali.
Moja ya mazao hayo ni pamoja na maharagwe machanga, maarufu kama Green
beans au French beans.
Utayarishaji wa shamba
Lima shamba na kuondoa magugu yote. Hakikisha
kuwa umelima kwa kiwango ambacho udongo umelainika
vya kutosha. Kabla ya kupanda ni lazima uhakikishe udongo umelainika
vizuri na una maji ya kutosha siku mbili kabla ya kupanda. Hii
inatege-meana na aina ya umwagiliaji, kwenye kilimo cha maharagwe
machanga inapendekezwa zaidi kutumia umwa-giliaji wa matone.
Kupanda
Inashauriwa kuweka nafasi ya sentim-ita 30 kati ya mstari na mstari, na
kati ya mmea na mmea sentimita 7. Panda mbegu moja kwa kila shimo.
Panda kwenye tuta na liwe na upana wa sen-timita 70, kati ya tuta na
tuta kuwepo nafasi ya sentimita 80. Ni vizuri kuacha nafasi ya
sentimita 15 kutoka pembeni mwa tuta unapo-panda mbegu, ili kuepusha
athari zin-azoweza kutokea na kuathiri mbegu au mmea baada ya kuota,
mfano, mafu-riko. Endapo unatumia umwagiliaji wa mifereji inashauriwa
kutengeneza makingo yenye kimo cha sentimita 15 na upana wa sentimita 70
kutoka kingo hadi kingo. Hii itasadia mimea kupata unyevu kwa urahisi
pamoja na kinga ya magonjwa yanayosababishwa na unyevu uliopitiliza.
Kupanda
Inashauriwa kutumia mbolea ya kupandia zinazotokana na miamba kama vile
DAP. Tumia gramu 5 kwa kila shimo. Hii itasaidia mizizi kuota kwa
haraka. Usifukie mbegu kwa zaidi ya inchi 1.5.
Mbegu za maha-ragwe machanga huota baada ya siku Mbegu Inapendekezwa
kutumia chotara aina ya F1. Aina hii ya mbegu imeonekana kuwa na
mafani-kio makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na uwezo wa kumudu
magonjwa. Inapendekezwa kupata mbegu kutoka kwa wazalishaji
walioidhin-ishwa.Aina za mbegu na uwezo wake?
Boston:
Aina hii ya mbegu ina uwezo mkubwa wa
uzalishaji. Wakati wa mvua aina hii ya mbegu husham-buliwa zaidi na
magonjwa hasa ya ukungu.?
Serengeti: Aina hii ina uzalishaji wa wastani. Aina hii ina uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa.?
Serengeti: Aina hii ina uzalishaji wa wastani. Aina hii ina uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa.?
Tana:
Aina hii uzalishaji wake ni mkubwa na wa
muda mrefu. Inashambuliwa na magonjwa kwa wastani. Aina hii huhitaji
kiwango kikubwa cha maji hasa wakati wa mavuno.Maharagwe machanga
yamegawa-nyika katika makundi mawili;?
Maharagwe mateke kwa wastani (fine beans) na?Maharagwe mateke zaidi (extra fine beans)wataalamu walio karibu nawe.
Maharagwe mateke kwa wastani (fine beans) na?Maharagwe mateke zaidi (extra fine beans)wataalamu walio karibu nawe.
Epuka maharagwe kugusana na maji au tope wakati wa kuvuna kwani inaweza kusababisha ugonjwa wa kuvunda, hivyo kupata hasara.
Baada ya kuvuna weka kwenye chombo chenye matundu kwa ajili ya kupitisha hewa. Hii ni wakati wa kuvuna kutoka shambani. Baada ya hapo, maharagwe yawekwe kwenye kreti maalumu na kuwekwa sehemu yenye ubaridi kusubiria uchambuzi na kuwekwa kwenye madaraja pamoja na kufungashwa.
Baada ya kuvuna weka kwenye chombo chenye matundu kwa ajili ya kupitisha hewa. Hii ni wakati wa kuvuna kutoka shambani. Baada ya hapo, maharagwe yawekwe kwenye kreti maalumu na kuwekwa sehemu yenye ubaridi kusubiria uchambuzi na kuwekwa kwenye madaraja pamoja na kufungashwa.
Endapo mbegu hazikuota vizuri unaweza kurudishia si zaidi ya siku mbili tangu maharagwe yaote.UmwagiliajiHii inategemeana na hali ya hewa/msimu, kulingana na eneo ulipo. Kwa kawaida maharagwe haya hustawi kwenye udongo usiotuamisha maji, na iwe kwenye ukanda wenye baridi ya wastani.
Utunzaji
Inapendekezwa kuwasiliana na mtaal-amu wa kilimo alie karibu nawe baada
ya siku 14 ili kufanya ukaguzi sham-bani kuona kama kuna dalili zozote
za wadudu pamoja na magonjwa kama vile mnyauko fuzari, endapo kuna
dalili zozote shauriana na mtaalamu. Mkulima anaweza kutumia mbolea
kwa ajili ya kukuzia na kurutubisha majani kulingana na mahitaji.
Ni lazima kupanda mahindi kuzun-guka shamba la maharagwe ili kuzuia
upepo unaoweza kuharibu maharagwe yako na yasiwe na ubora unaotakiwa.
Palizi Ni muhimu kufanya palizi kuanzia baada ya siku kumi ili kuepusha
makazi/maficho ya wadudu wahari-bifu. Unaweza kunyunyiza dawa ya kuzuia
kutu baada ya wiki tatu.
Maharagwe machanga huchukua wiki 9-10 tangu kupanda hadi kuvuna. Hii
inategemeana na hali ya hewa pamoja na mbegu. Maharagwe haya huchanua
baada ya wiki sita. Wakati huu mkulima anatakiwa kuwa makini sana
kutokana na uwezekano wa kuwepo wadudu waharibifu kama vile thiripi.
Inapende-kezwa kuwasiliana kwa karibu na mta-alamu wa kilimo ili kufanya
ukaguzi ili kubaini aina ya wadudu na hatua za kuchukua.
Uvunaji:
Maharagwe machanga
yanafaa kuvunwa viriba vinapokuwa na urefu wa sentimita 11.5-15, unene
wa mil-imita 6-8. Hii hufanyika katika wiki ya 9-10.
Kwa kuanzia, hapo juu ni maelezo mafupi juu ya kilimo hiki.
0 comments:
Post a Comment