Pilipili
hoho ni moja ya mazao ya viungo
ambalo hulimwa kwa wingi Mikoa
ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro,
Mbeya na Iringa.
Zao hili
hutumika kama kiungo kwenye
vyakula mbalimbali kama vile vyama,
viazi na ndizi. Vilevile hutumika
katika kutengeneza kachumbari na
kuweza kukaushwa na kusagwa ili kupata
unga.
Viini lishe
vinavyopatikana katika pilipili tamu
au hoho ni Vitamini A,B,C na
madini aina ya chokaa na chuma.
MAZINGIRA:
Zao
hili hukua vizuri kwenye hali
ya hewa yenye joto la wastani
(nyuzi joto 18 hadi 20) za
Sentigredi, joto likizidi vichomozo,
maua na matunda huanguka.
Huhitaji
mwinuko wa kuanzia usawa
wa bahari hadi mita 1,500
na mvua za wastani kiasi cha
milimita 600 hadi 1500.
Udongo
unaofaa kwa zao hili ni
ule wenye rutuba, mboji nyingi,
kina kirefu na usiotuamisha maji.
AINA:
Kuna aina
nyingi za pilipili hoho. Baadhi ya
aina zinazostawishwa nchini ni
California, Wonder, Emerald Giant,
Sweet Neapotitan, Yolo Wonder,
Pimiento na Keystone Resistant
Giant. Aina zingine ni kama
vile Ruby King, Ruby
Giant, Libert Bell na Yolo
Wonder B.
KUPANDA MBEGU:
Mbegu
zinaweza kupandwa moja kwa
moja shambani au kuoteshwa
kwanza kwenye kitalu na baadaye
kuhamishiwa shambani.
Kuotesha mbegu
Kitaluni.
Kabla ya
kusia mbegu tengeneza tuta
lenye upana wa mita moja.
Urefu wa tuta utategemea eneo la shamba
linalotarajiwa kupandwa. Weka mbolea
za asili zilizooza vizuri kiasi
cha ndoo mbili au zaidi
katika eneo la mita mraba
moja. Changanya mbolea na
udongo vizuri, kisha tengeneza
vifereji vyenye nafasi ya
sentimeta 10 hadi 15 kutoka
kifereji hadi kingine. Kina cha
kifereji kiwe sentimeta moja
hadi tatu katika eneo hilo,
kiasi hiki kitatoa miche ambayo
itatosha kupandikiza katika eneo la
mita mraba 100.
Baada ya kusia
fukia kwa kutumia udongo laini au
mbolea za asili zilizooza vizuri.
Weka matandazo na kisha
mwagilia maji. Endelea kumwagilia
kitalu kila siku asubuhi na
jioni hadi mbegu zitakapoota.
Mbegu huota baada ya siku
sita hadi 10. Mara
zitakapoota ondoa matandazo. Endelea
kumwagilia maji hadi wakati miche
inakuwa tayari kwa kupandikizwa.
KUTAYARISHA SHAMBA
Tayarisha
shamba vizuri mwezi mmoja kabla
ya kupandikiza miche, katua ardhi
katika kina cha kutosha sentimeta 30
kwenda chini, weka mbolea za
asili kiasi cha tani 10
hadi 15 kwa hekta. Kiasi
hiki ni sawa na debe moja
kwa eneo la mita mraba moja
changanya mbolea na udongo
vizuri.
Ikiwa eneo
hilo lina upungufu wa madini
aina ya fosiforasi kama itakavyothibitishwa
na wataalam, weka mbolea ya
chokaa aina ya TSP. Kiasi
kinachotakiwa ni kilo 200 kwa
hekta. Lainisha udongo siku tatu
au tano kabla ya kupandikiza
miche.
KUPANDIKIZA MICHE:
Miche huwa
tayari kwa kupandikizwa shambani
baada ya wiki nne hadi
10. Wakati huu huwa
na majani sita hadi manane na
urefu wa sentimeta 10 hadi 15.
Pandikiza
miche katika nafasi ya
sentimeta 40 hadi 50 kutoka shimo
hadi shimo na sentimeta 60 hadi
75 kati ya mstari na mstari.
Ikiwa mbolea za asili
hazikuwekwa wakati wa
kutayarisha shamba, weka kiasi cha
nusu kilo hadi moja
katika kila shimo la
kupandia.
Siku moja
kabla ya kung’oa miche,
mwagilia tuta ili kulainisha udongo.
Ng’oa miche pamoja na udongo
wake kisha pandikiza katika kina
cha sentimita mbili zaidi kuliko
ilivyokuwa kwenye kitalu. Pandikiza
miche wakati wa asubuhi au
jioni. Mara baada ya
kupandikiza mwagilia maji ya kutosha.
KUTUNZA SHAMBA
·
Kuweka matandazo.
Tandaza nyasi kavu
ili kuhifadhi unyevu ardhini,
kuongeza rutuba ya
udongo, kuzuia uotaji wa
magugu, na mmmomonyoko wa ardhi.
·
Palizi.
Palilia shamba kila
magugu yanapoota. Wakati wa kupalilia
pandishia udongo kuzunguka shina ili
kuifunika mizizi, na kuzuia
mmea usiangushwe na upepo mkali.
·
Kumwagilia Maji.
Pilipili hoho hustawi
vizuri iwapo zimepata maji ya
kutosha. Hivyo umwagiliaji wa
mara kwa mara hasa wakati
wa kiangazi ni wa muhimu.
·
Kuweka Mbolea.
Zao hili huhitaji
mbolea za kukuzia. Hizi
ni kama mbolea ya S/A, CAN, Urea na
mbolea ya mchanganyiko aina ya
N.P.K Mbolea ya mchanganyiko (N.P.K)
huwekwa wakati maua yanapoanza
kutoka. Kiasi kinachowekwa ni
gramu tisa hadi 10
(kijiko kimoja kikubwa) kwa kila
mmea. Majuma manne baadaye
weka CAN, S/A au
Urea. Weka gramu sita
(kijiko kidogo cha chai) kwa
kila mche, kama utatumia CAN au
S/A. ikiwa utatumia Urea, weka
gramu tatu ( nusu kijiko cha
chai) kwa kila mche).
Wadudu waharibifu na Magonjwa.
Wadudu.
·
Vidukari au
wadudu Mafuta ( Aphids).
Hivi ni vijidudu vidogo
vyenye rangi nyeusi,
kijani au kahawia.
Hushambuliwa majani kwa
kufyonza utomvu wake na
kusababisha mmea kudumaa.
Vidukari huzuiwa kwa
kunyunyizia dawa kama vile
Dimothoate au Selecron.
·
Mbawakau.
Ni wadudu wenye rangi
nyeusi iliyochanganyika na kahawia.
Mabawa yao kwa nje ni
magumu. Hushambulia shina
karibu na usawa wa ardhi na
kulifanya liwe na nundu.
Zuia wadudu hawa kwa
kutumia mojawapo ya dawa
zifuatazo; Carbaryl, au Dimecron.
·
Fukusi wa
Pilipili (Pepper Weevil)
Mdudu huyu ni hatari
sana kwa zao hili na mashambulizi
kufanywa na funza wake wenye rangi
nyeupe. Funza hawa hula sehemu
ya ndani ya vichomozo na
matunda machanga nan
kusababisha kuanguka. Angamiza wadudu
hawa kwa kutumia moja ya
dawa zifuatazo; Actellic, Sumithion
au Carbaryl.
·
Vithiripi (Thrips)
Hivi ni vijidudu vidogo
vyenye rangi ya njano.
Hushambulia majani na husababisha mmea
kuwa na rangi nyeupe
yenye kung’aa. Mmea pia kunyauka
kuanzia kwenye ncha ya
jani. Vijidudu hivi pia kueneza
magonjwa yatokanayo na virusi.
Zuia vijidudu hivi
kwa kutumia dawa kama vile;-
Cyrmethrin, Sumicidin au Dimercon.
·
Sota (Cutworms)
Hawa hukata miche
michanga karibu na usawa wa
ardhi. Ili kuwazuia wadudu hawa,
tumia dawa kama vile
Carbaryl, Sumicidin au
Ekalux. Nyunyizia mara
baada ya kupandikiza.
·
Inzi Weupe
(White flies).
Ni vidudu vidogo
vyenye rangi nyeupe, na
huonekana kama vumbi la
unga vikiwa kwenye majani.
Mmea ukitikiswa huruka.
Hushambulia mmea kwa
kufyoza utomvu wake, na
hueneza ugonjwa wa virusi
unaosababisha kujikunja kwa majani.
Inzi weupe wanaweza
kuzuiwa kwa kutumia Sumicidin,
Sapa Diazinon au Diclorvos.
·
Utiriri
Mwekundu (Red Spidermites)
Hawa ni wadudu wadogo
wenye rangi nyekundu au rangi
ya machungwa yaliyoiva. Huonekana
upande wa chini wa majani
na hushambulia mmea kwa kufyonza
utomvu wake.
Zuia utitiri kwa kutumia
dawa kama vile Kelthane, Dimethoate
na Diazinon.
Magonjwa
·
Magonjwa ya
Virusi
Magonjwa haya hutokana
na virusi. Husababisha majani
kudumaa, kukunjamana, na kuwa
na rangi ya njano. Ili
kuzuia magonjwa haya, zingatia yafuatazo;-
-
Panda
aina ya pilipili zinazostahimili
mashambulizi j ya magonjwa haya.
-
Ng’oa
miche inayoonyesha dalili za
magonjwa haya.
-
Zuia wadudu
wanaoeneza magonjwa ya virusi kwa
kutumia dawa ya Kelthane 30 E,
C, Dimethoate, Diazinon na Ekalux.
-
Badilisha
mazao. Baada ya
kuvuna pilipili tamu, zao
linalofuata lisiwe la jamii la zao
hili kwa mfano nyanya na
bilinganya.
Chule (Anthracnose)
Ugonjwa huu
husababishwa na ukungu. Hushambulia
matunda na kuyasababisha kuwa na makovu j
ya mviringo yenye rangi nyeusi
iliyochanganyika na kahawia.
Zuia ugonjwa huu kwa
kunyunyizia mojawapo ya dawa zifuatazo:
Dithane - M 45, Topsini - M,
Ridomol au Kocide,
·
Madoa
Bakteria (Bacterial Leaf spot)
Ugonjwa huu
husababishwa na viini vya vya
bacteria. Hushambulia majani machanga j na
baadaye matunda. Dalili j zake ni kuonekana
kwa madoa ya njano kwenye majani
na matunda.
Zuia ugonjwa
huu hkwa kupanda mbegu zilizothibitishwa na
wataalam.
·
Kuoza Mizizi
(Root Rot)
Huu ni ugonjwa wa
ukungu unaoshambulia mizizi na
kusababisha kuoza. Mmea
hunyauka na hatimaye hufa. Ugonjwa huu
hupendelea sana hali ya unyevunyevu
na joto jingi, hivyo zuia
hali hii kwa kuepuka kupanda pilipili
kwenye sehemu h inayotuamisha maji.
Hali ikiwa mbaya, tumia dawa
za ukungu h kama vile Dithane M 45,
Tpsin - M 70 au Ridomil.
·
Mnyauko
Verticilium (Verticilim Wilt)
Huu pia ni ugonjwa
unaoletwa na ukungu ambao
hupatikana kwenye udongo. Hushambulia
shina na kulisababisha libadilike rangi na
kuwa ya kahawia. Baadaye mmea
hunyauka na kufa. Unaweza kuzuia
ugonjwa huu kwa kubadilisha mazao.
KUVUNA
Pilipili hoho huwa tayari
kwa kuvunwa baada ya wiki 10 hadi 14
tangu kupandikiza miche. Uvunaji
huendelea kwa muda wa wiki nane
hadi 10. Muda wa kuvuna hutegemea
aina na matumizi. Pilipili kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani
huvunwa zingali na rangi yake
ya kijani kibichi inayong’aa . zile
za kisindika kiwandani
huvunwa zikiwa zimekomaa na zenye
rangi nyekundu. Matunda yakivunwa
tangali machanga hunyauka kwa urahisi,
kusinyaa na hupunguza wingi wa
mazao. Wastani wa mavuno huwa
kwa hekta ni tani 30 hadi 45.
SOMA MAKALA NYINGINE ZA KILIMO HAPA
SOMA MAKALA NYINGINE ZA KILIMO HAPA
0 comments:
Post a Comment