• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Monday, September 26, 2016

FAHAMU KILIMO BORA CHA ZAO LA UFUTA


UFUTA   (Sesamum indicum)


UTANGULIZI
         Ufuta (simsim/sesame) ni zao la kibiashara ambalo mbegu zake zina kiasi kikubwa cha mafuta kiasi cha asilimia 45 hadi 55.Na zao hili linaweza kulimwa maeneo mengi ya Afrika mashariki  na Tanzania.Ni zao ambalo linatowa mafuta yenye thamani kubwa na hivyo kulifanya zao bora la biashara.

HALI YA HEWA  INAYOFAA KWA KILIMO CHA UFUTA

 Zao hili linawezwa kulimwa katika maeneo yanayopata mvua kidogo.Maeneo ya ukanda wa chini  usawa wa bahari hufaa zaidi kwa kilimo cha ufuta.Pia nyanda za juu ambazo ni chini ya mita 1500 hufaa kwa kilimo cha ufuta.Mfano kwa Tanzania unaweza Ukalima ufuta katika mikoa ya Morogoro,Lindi,Manyara,Dodoma,Iringa.


UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA UFUTA

Ufuta ustawi vizuri katika maeneo yenye udongo mwepesi mweusi na usiotuamisha maji,udongo tifutifu ni mzuri kwa kilimo cha ufuta,Pia ufuta unawezwa kulimwa katika udongo wowote lakini usiotuamisha maji.Ufuta hufa haraka kama maji yatatuama kwa muda mrefu shambani.

AINA ZA UFUTA

Kuna aina kuu mbili za mbegu za ufuta:

1) MBEGU ZA ASILI
     Wakulima wengi hupanda mbegu za asili, mbegu ambazo zilianza kulimwa miaka mingi iliyopita.Mbegu hizi nyingi zina mavuno kidogo na huchukua muda mrefu kukomaa Huchukua siku 140 hadi 180.

2) MBEGU ZA KISASA
     Mbegu hizi zinakomaa kwa muda mfupi na hutowa mavuno mengi, wastani wa kilogram 500 hadi 800 kwa ekari kama shamba litaandaliwa litapandwa na litatunzwa vizuri.Mbegu hizi huchukua siku 105 hadi 140 kukomaa.Mfano wa mbegu hizi ni Naliendele 92,Lindi 202,Ziada 94 na Mtwara 2009.

UPANDAJI WA UFUTA

Shamba la ufuta ni budi likatuliwe na kulimwa vizuri kabla ya kupanda,hata hivyo pia unaweza kupanda bila kukatua lakini mavuno yatapungua kidogo.Inashauriwa kupanda ufuta kwa mistari kwa vipimo vifuatavyo.Sentimeta 50 kwa 10 au 50 kwa 20 kama utapanda kwa kutumia mistari ya kuchimba vijifereji vidogo katika mstari na kudondosha mbegu hizo katika vifereji hivyo (Drilling method) na kwa kuacha mche mmoja mmoja kwa kila shina.
Pia sentimeta 50 kwa 30  au 60 kwa 30 kwa kuacha miwili kwa kila shina. Kwa Mbegu ya Asili Unaweza Kupanda kwa sentimeta 70 kwa 30 kwa Kuacha Miwili kwa Kila shimo.Fukia mbegu kwa sentimenta .2.5 hadi 5.

MUDA WA KUPANDA

Muda mzuri wa kupanda ufuta ni mwanzoni mwa msimu wa kilimo  yaani Mwishoni mwa mwezi Desemba hadi katikati kwa mwezi Januari.

MATUMIZI YA MBOLEA

Ufuta ni zao ambalo halihitaji matumizi makubwa ya Mbolea.Japokuwa hustawi zaidi katika udongo wenye rutuba ya kutosha.Kama utapanda katika ardhi isiyo na rutuba ya kutosha basi unaweza kutumia mbolea kiasi kidogo Mbolea kama vile UREA na BUSTA.

MATUNZO NA PALIZI

 Miche ya ufuta ni midogo na laini sana hivyo inahitaji palizi mapema hasa katika kipindi cha majuma manne ya kwanza .Pia katika kipindi hiki unatakiwa kupunguza miche iliyosongamana.Kadri utavyochelewesha palizi na kupunguzia mimea mapema ndivyo unavyoifanya mimea isikuwe vizuri na kujipunguzia kipato chako.

MAGONJWA YA UFUTA

Magonjwa makuu ya ufuta ni madoa ya majani na kuoza matawi na shina.Zuia magonjwa haya kwa Kupanda  mbegu bora  na kwa kutokupanda ufuta katika ardhi inayotuamisha  maji,pia itawezekana kubadilisha shamba usilime  ufuta katika shamba lililolimwa msimu uliopita.


WADUDU WANAOSHAMBULIA UFUTA

  Kuna wadudu wengi wanaoshambulia ufuta kama vile vibaruti (Ambao hushambulia hatua ya mwanzo kabisa ya miche iliyoota ya ufuta  ambapo vibaruti hula majani ya mwanzo ya mmea mara tu yanapojitokeza).Pia Aphidi hushambulia ufuta kwa kufyonza maji katika majani ya mimea hivyo kupelekea kukauka kwa majani ya mmea.
  Pia wapo funza wa majani ambao hula majani ya mimea na pia hufunga majani ya ncha ya mimea na kuzuia ukuaji wa matawi wa mimea,wadudu hawa ni hatari zaidi kwani wanazuia kutengenezwa kwa vitumba vya ufuta.
  Kuzuia vibaruti,kabla hujapanda mbegu yako changanya na dawa ya tunza au gaucho.Pia panda mbegu bora na fanya mzunguko mazao shambani.Wadudu wengine wakijitokeza tumia dawa kama karate,dimethoate.Twigathoate,duduall,duduba  na dawa nyingine za wadudu kabla wadudu hawajasababisha madhara makubwa shambani.

UVUNAJI

  Ufuta uliokomaa tayari kwa kuvunwa utaonesha mabadiliko ya majani yake na shina na matawi yatabadilika  rangi yake na kuwa njano au kahawia au yataanza kukauka,pia vitumba vya mwanzo vitaanza kubadilika rangi yake na kuanza kukauka hivyo utatakiwa ukate ufuta mapema kabla vitumba havijakauka na kupasuka.Vuna ufuta wako kwa kukata matawi ya ufuta  na kuyafunga katika matita ya saizi inayokufaa ila yasiwe matita makubwa sana ambayo hayatakauka katikati kwa urahisi yasimamishe matita yako kuelekeza juu kisha acha yakauke kwa wiki mbili hadi nne kutegemea na ukali wa jua.vitumba vikisha kauka na kupasuka tandika mkeka au turubai na yageuze matita yako katika mkeka na turubai hapo ufuta utamwagikia katika mkeka au turubai lako,kuupata ufuta unaokwama katika matita piga piga kidogo tita unapoligeuza.Kisha Peta ufuta wako na kuuweka katika Vyombo safi vya kuhifadhia.


                                        Picha mbalimbali za ufuta shambani







Share:

FAHAMU KILIMO BORA CHA PILIPILI NA FAIDA ZAKE




Pilipili   hoho  ni  moja  ya  mazao   ya  viungo  ambalo  hulimwa  kwa   wingi    Mikoa  ya   Arusha,  Kilimanjaro,  Tanga,  Morogoro, Mbeya  na   Iringa.

Zao   hili   hutumika    kama  kiungo   kwenye  vyakula   mbalimbali  kama  vile  vyama,   viazi  na  ndizi.    Vilevile    hutumika   katika  kutengeneza   kachumbari   na  kuweza  kukaushwa   na  kusagwa   ili  kupata   unga.

Viini  lishe   vinavyopatikana    katika  pilipili    tamu au hoho  ni  Vitamini   A,B,C  na  madini   aina  ya  chokaa  na  chuma.

MAZINGIRA:
Zao   hili    hukua  vizuri  kwenye  hali  ya  hewa   yenye  joto  la  wastani   (nyuzi  joto   18  hadi  20)   za  Sentigredi,  joto  likizidi   vichomozo,   maua  na  matunda   huanguka.

Huhitaji    mwinuko   wa  kuanzia   usawa  wa    bahari   hadi  mita  1,500  na  mvua   za  wastani  kiasi  cha  milimita   600  hadi  1500.

Udongo   unaofaa   kwa  zao  hili   ni  ule   wenye    rutuba,  mboji  nyingi,  kina  kirefu  na   usiotuamisha  maji.

AINA:
Kuna  aina   nyingi  za  pilipili  hoho.   Baadhi ya  aina   zinazostawishwa   nchini   ni  California,  Wonder,   Emerald    Giant,  Sweet  Neapotitan,   Yolo   Wonder,  Pimiento  na  Keystone   Resistant   Giant.   Aina  zingine   ni  kama  vile    Ruby  King,   Ruby    Giant,   Libert   Bell  na   Yolo  Wonder  B.

KUPANDA   MBEGU:
Mbegu   zinaweza    kupandwa  moja  kwa   moja   shambani  au   kuoteshwa   kwanza   kwenye  kitalu  na  baadaye   kuhamishiwa   shambani.



Kuotesha   mbegu  Kitaluni.
Kabla    ya  kusia   mbegu   tengeneza   tuta  lenye   upana   wa  mita  moja.   Urefu  wa  tuta   utategemea  eneo  la  shamba   linalotarajiwa  kupandwa.   Weka  mbolea   za  asili  zilizooza    vizuri  kiasi  cha  ndoo  mbili   au   zaidi  katika   eneo  la  mita  mraba   moja.    Changanya  mbolea   na  udongo  vizuri,   kisha   tengeneza    vifereji  vyenye   nafasi  ya    sentimeta  10  hadi  15  kutoka   kifereji   hadi   kingine.   Kina  cha  kifereji   kiwe  sentimeta   moja  hadi     tatu  katika  eneo  hilo,  kiasi  hiki  kitatoa   miche    ambayo  itatosha  kupandikiza  katika  eneo   la  mita  mraba  100.

  
Baada  ya  kusia  fukia kwa  kutumia   udongo  laini  au  mbolea  za  asili    zilizooza  vizuri.  Weka    matandazo      na  kisha   mwagilia  maji.   Endelea   kumwagilia   kitalu  kila  siku   asubuhi  na  jioni   hadi  mbegu   zitakapoota.    Mbegu   huota   baada  ya  siku  sita   hadi  10.   Mara   zitakapoota   ondoa   matandazo.   Endelea  kumwagilia  maji   hadi  wakati   miche  inakuwa   tayari   kwa  kupandikizwa.

KUTAYARISHA   SHAMBA
Tayarisha   shamba   vizuri   mwezi   mmoja kabla  ya  kupandikiza  miche,   katua   ardhi  katika  kina  cha  kutosha  sentimeta   30  kwenda  chini,    weka  mbolea  za  asili   kiasi  cha   tani  10  hadi   15   kwa  hekta.  Kiasi  hiki   ni sawa  na  debe   moja   kwa  eneo   la  mita  mraba  moja  changanya    mbolea  na  udongo   vizuri.   

Ikiwa   eneo  hilo   lina   upungufu   wa  madini  aina  ya  fosiforasi  kama  itakavyothibitishwa  na  wataalam,    weka  mbolea     ya  chokaa  aina  ya   TSP.   Kiasi   kinachotakiwa   ni  kilo  200  kwa  hekta.   Lainisha   udongo  siku  tatu  au  tano  kabla   ya   kupandikiza   miche.

KUPANDIKIZA   MICHE:
Miche   huwa   tayari  kwa  kupandikizwa   shambani   baada  ya  wiki   nne  hadi  10.    Wakati   huu     huwa  na  majani  sita  hadi  manane   na  urefu   wa   sentimeta   10  hadi  15.

Pandikiza   miche   katika  nafasi    ya   sentimeta   40  hadi  50  kutoka  shimo  hadi  shimo  na  sentimeta 60    hadi  75  kati  ya   mstari  na  mstari.   Ikiwa    mbolea   za  asili   hazikuwekwa    wakati  wa    kutayarisha   shamba,  weka  kiasi  cha  nusu  kilo   hadi   moja   katika    kila  shimo  la   kupandia.   

Siku   moja  kabla  ya  kung’oa   miche,   mwagilia   tuta   ili   kulainisha   udongo.    Ng’oa   miche  pamoja   na   udongo  wake   kisha   pandikiza  katika  kina  cha   sentimita   mbili   zaidi   kuliko   ilivyokuwa  kwenye  kitalu.   Pandikiza   miche  wakati  wa  asubuhi  au  jioni.    Mara  baada  ya  kupandikiza   mwagilia  maji   ya  kutosha.


KUTUNZA   SHAMBA
·         Kuweka   matandazo.
Tandaza    nyasi   kavu  ili  kuhifadhi   unyevu  ardhini,  kuongeza   rutuba   ya   udongo,    kuzuia   uotaji   wa  magugu,   na   mmmomonyoko   wa  ardhi.


·        Palizi.
Palilia   shamba  kila   magugu   yanapoota.   Wakati  wa  kupalilia  pandishia  udongo  kuzunguka   shina  ili  kuifunika   mizizi,  na   kuzuia   mmea   usiangushwe  na   upepo   mkali.

·        Kumwagilia   Maji.
Pilipili   hoho   hustawi   vizuri   iwapo  zimepata   maji  ya  kutosha.    Hivyo   umwagiliaji   wa  mara  kwa   mara  hasa    wakati   wa  kiangazi  ni  wa  muhimu.

·        Kuweka   Mbolea.
Zao    hili   huhitaji   mbolea     za  kukuzia.   Hizi  ni  kama  mbolea  ya  S/A,  CAN,  Urea  na  mbolea   ya  mchanganyiko   aina  ya  N.P.K  Mbolea  ya  mchanganyiko  (N.P.K)  huwekwa   wakati  maua  yanapoanza   kutoka.   Kiasi  kinachowekwa   ni   gramu   tisa  hadi  10     (kijiko  kimoja  kikubwa)   kwa  kila  mmea.   Majuma  manne   baadaye   weka   CAN,   S/A  au   Urea.    Weka  gramu  sita   (kijiko   kidogo  cha  chai)    kwa  kila  mche,    kama  utatumia  CAN  au  S/A.  ikiwa    utatumia   Urea,  weka  gramu   tatu  (  nusu   kijiko  cha  chai)  kwa  kila  mche).



Wadudu   waharibifu   na  Magonjwa.
Wadudu.
·         Vidukari  au  wadudu   Mafuta   (  Aphids).
Hivi  ni  vijidudu   vidogo   vyenye   rangi   nyeusi,   kijani    au  kahawia.   Hushambuliwa     majani  kwa  kufyonza   utomvu  wake  na    kusababisha  mmea  kudumaa.

Vidukari   huzuiwa  kwa  kunyunyizia  dawa   kama  vile   Dimothoate   au   Selecron.


·         Mbawakau.
Ni  wadudu   wenye  rangi   nyeusi  iliyochanganyika   na  kahawia.   Mabawa   yao  kwa  nje  ni   magumu.    Hushambulia   shina   karibu   na  usawa  wa  ardhi   na  kulifanya  liwe  na   nundu.

Zuia  wadudu   hawa  kwa  kutumia   mojawapo   ya   dawa  zifuatazo;  Carbaryl,   au   Dimecron.

·        Fukusi   wa   Pilipili   (Pepper    Weevil)
Mdudu  huyu  ni  hatari   sana  kwa  zao  hili  na  mashambulizi   kufanywa  na  funza  wake   wenye  rangi  nyeupe.   Funza   hawa  hula   sehemu  ya   ndani  ya  vichomozo   na  matunda   machanga   nan   kusababisha   kuanguka.   Angamiza   wadudu   hawa   kwa   kutumia  moja   ya  dawa  zifuatazo;   Actellic,   Sumithion  au  Carbaryl.

·        Vithiripi   (Thrips)
Hivi  ni  vijidudu   vidogo   vyenye   rangi  ya   njano.   Hushambulia   majani  na  husababisha  mmea  kuwa  na    rangi   nyeupe   yenye   kung’aa.  Mmea   pia  kunyauka  kuanzia  kwenye   ncha  ya   jani.    Vijidudu  hivi  pia   kueneza  magonjwa   yatokanayo  na virusi.

Zuia   vijidudu   hivi   kwa  kutumia   dawa  kama  vile;-   Cyrmethrin,  Sumicidin  au   Dimercon.


·        Sota  (Cutworms)
Hawa   hukata  miche   michanga   karibu  na  usawa   wa  ardhi.  Ili  kuwazuia  wadudu   hawa,  tumia   dawa  kama   vile   Carbaryl,    Sumicidin  au   Ekalux.    Nyunyizia     mara   baada  ya   kupandikiza.
·         Inzi   Weupe  (White   flies).
Ni   vidudu   vidogo   vyenye   rangi   nyeupe,  na    huonekana  kama     vumbi  la   unga   vikiwa   kwenye  majani.   Mmea   ukitikiswa   huruka.
Hushambulia   mmea   kwa  kufyoza     utomvu  wake,   na  hueneza   ugonjwa  wa  virusi    unaosababisha   kujikunja   kwa  majani.
Inzi   weupe  wanaweza  kuzuiwa    kwa  kutumia   Sumicidin,  Sapa  Diazinon  au   Diclorvos.

·        Utiriri   Mwekundu   (Red   Spidermites)
Hawa  ni  wadudu   wadogo   wenye   rangi   nyekundu  au  rangi  ya  machungwa   yaliyoiva.   Huonekana  upande   wa  chini  wa   majani    na   hushambulia    mmea   kwa  kufyonza  utomvu  wake.
Zuia   utitiri   kwa  kutumia  dawa  kama  vile  Kelthane,   Dimethoate  na  Diazinon.
Magonjwa

·        Magonjwa   ya   Virusi
Magonjwa  haya   hutokana   na  virusi.   Husababisha   majani   kudumaa,    kukunjamana,   na  kuwa  na  rangi  ya   njano.     Ili  kuzuia  magonjwa  haya,  zingatia   yafuatazo;-
-           Panda   aina   ya  pilipili   zinazostahimili   mashambulizi j ya  magonjwa  haya.
-         Ng’oa     miche     inayoonyesha  dalili  za  magonjwa   haya.
-         Zuia   wadudu   wanaoeneza   magonjwa   ya  virusi  kwa  kutumia  dawa   ya  Kelthane  30  E,  C,  Dimethoate,  Diazinon  na  Ekalux.
-         Badilisha   mazao.   Baada   ya  kuvuna      pilipili  tamu,  zao   linalofuata   lisiwe  la  jamii  la  zao  hili    kwa  mfano    nyanya  na  bilinganya.
Chule   (Anthracnose)
Ugonjwa   huu  husababishwa  na  ukungu.   Hushambulia  matunda   na  kuyasababisha  kuwa  na  makovu j ya  mviringo  yenye rangi   nyeusi   iliyochanganyika  na  kahawia.

Zuia   ugonjwa  huu kwa kunyunyizia   mojawapo  ya dawa  zifuatazo:   Dithane   -  M  45, Topsini  -  M,   Ridomol  au    Kocide,  
·         Madoa  Bakteria   (Bacterial    Leaf   spot)
Ugonjwa   huu  husababishwa   na  viini  vya   vya  bacteria.   Hushambulia   majani  machanga j na  baadaye  matunda.   Dalili j zake  ni  kuonekana  kwa  madoa   ya  njano   kwenye majani  na  matunda.

Zuia   ugonjwa   huu hkwa  kupanda   mbegu  zilizothibitishwa  na  wataalam.

·         Kuoza  Mizizi  (Root   Rot)
Huu  ni   ugonjwa   wa  ukungu  unaoshambulia  mizizi  na  kusababisha    kuoza.    Mmea  hunyauka  na  hatimaye   hufa.  Ugonjwa   huu   hupendelea   sana  hali  ya  unyevunyevu  na  joto  jingi,   hivyo   zuia   hali  hii  kwa  kuepuka   kupanda  pilipili  kwenye   sehemu h inayotuamisha  maji.

Hali  ikiwa  mbaya,  tumia  dawa  za  ukungu h kama  vile  Dithane  M  45,  Tpsin  -  M   70   au   Ridomil.

·          Mnyauko    Verticilium   (Verticilim  Wilt)
Huu  pia   ni   ugonjwa   unaoletwa  na  ukungu   ambao   hupatikana   kwenye  udongo.   Hushambulia  shina  na  kulisababisha  libadilike  rangi  na  kuwa  ya  kahawia.  Baadaye   mmea   hunyauka  na  kufa.  Unaweza   kuzuia   ugonjwa  huu  kwa  kubadilisha  mazao.

KUVUNA 
Pilipili  hoho  huwa tayari  kwa  kuvunwa  baada  ya  wiki 10  hadi  14  tangu  kupandikiza  miche.   Uvunaji  huendelea    kwa  muda  wa  wiki  nane  hadi  10.   Muda  wa  kuvuna  hutegemea  aina   na  matumizi.  Pilipili   kwa  ajili  ya  matumizi  ya  nyumbani   huvunwa    zingali   na  rangi  yake  ya  kijani  kibichi    inayong’aa .  zile  za    kisindika   kiwandani   huvunwa   zikiwa  zimekomaa  na  zenye  rangi  nyekundu.   Matunda  yakivunwa   tangali  machanga   hunyauka  kwa  urahisi,  kusinyaa  na   hupunguza   wingi  wa  mazao.    Wastani  wa  mavuno  huwa  kwa  hekta   ni  tani  30  hadi   45.

SOMA MAKALA NYINGINE ZA KILIMO HAPA
Share:

Saturday, September 10, 2016

Fahamu Ufugaji Nyuki



Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.
Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.
Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.
VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-
UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.
DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-
1.      Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.
Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.
Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.
2.      Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.
3.      Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.
Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.
MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-
1.      Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-
a.      Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.
Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.
Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.
b.      Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.
c.       Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.
Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.
Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2.      Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.
Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.
Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.

PICHA ZA MABANDA TOFAUTI TOFAUTI YA KUFUGIA NYUKI
Picha 1:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa udongo maarufu kama tembe.
Picha 2:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi
Picha 3:Nyumba ya kufugia nyuki iliyojengwa kwa matofali na kuwekewa midomo maalumu ya nyuki kwa ajili ya kuingia na kutoka pindi wanapokwenda kutafuta chakula
Picha 4:Kibanda kidogo cha kisasa kwa jili ya kufugia nyuki.
Picha 5:Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa bati
Picha 6: Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti, kuezekwa kwa bati na kuwekewa uzio wa waya.
Share:

Monday, September 5, 2016

FAHAMU KILIMO CHA TANGAWIZI





Kwa ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawiz zinastawi.
KUANDAA SHAMBA

Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA

Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia  mbolea ya mboji au samadi na usitumie  mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara  Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.
MAGONJWA

Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).
KUVUNA

Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
 Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka
 Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawiz unaweza kusubir soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka
 Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali
Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzàlisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata  uzoefu kupitia hapo na kujua kama  eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawiz.
 Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg.
 Usikatishe tamaa pale  tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka
 HALI YA HEWA

Mimea hii husitawi katika maeneo  yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.
Share:

FAHAMU KILIMO CHA MAHARAGWE MACHANGA/GREEN BEANS


maharagwe machanga yakiwa tayari yamevunwa


Hivi karibuni hapa nchini Tanzania, kumekuwa na uanzishaji na uendelezaji wa kilimo cha mazao mapya ambayo hayakuzoeleka hapo awali.   Moja ya mazao hayo ni pamoja na maharagwe machanga, maarufu kama Green beans au French beans.
Utayarishaji wa shamba
Lima shamba na kuondoa magugu yote. Hakikisha
kuwa umelima kwa kiwango ambacho udongo umelainika vya kutosha. Kabla ya kupanda ni lazima uhakikishe udongo umelainika vizuri na una maji ya kutosha siku mbili kabla ya kupanda. Hii inatege-meana na aina ya umwagiliaji, kwenye kilimo cha maharagwe machanga inapendekezwa zaidi kutumia umwa-giliaji wa matone.
Kupanda
Inashauriwa kuweka nafasi ya sentim-ita 30 kati ya mstari na mstari, na kati ya mmea na mmea sentimita 7. Panda mbegu moja kwa kila shimo.
Panda kwenye tuta na liwe na upana wa sen-timita 70, kati ya tuta na tuta kuwepo nafasi ya sentimita 80.     Ni vizuri kuacha nafasi ya sentimita 15 kutoka pembeni mwa tuta unapo-panda mbegu, ili kuepusha athari zin-azoweza kutokea na kuathiri mbegu au mmea baada ya kuota, mfano, mafu-riko. Endapo unatumia umwagiliaji wa mifereji inashauriwa kutengeneza makingo yenye kimo cha sentimita 15 na upana wa sentimita 70 kutoka kingo hadi kingo. Hii itasadia mimea kupata unyevu kwa urahisi pamoja na kinga ya magonjwa yanayosababishwa na unyevu uliopitiliza.
Kupanda
Inashauriwa kutumia mbolea ya kupandia zinazotokana na miamba kama vile DAP. Tumia gramu 5 kwa kila shimo. Hii itasaidia mizizi kuota kwa haraka. Usifukie mbegu kwa zaidi ya inchi 1.5.
Mbegu za maha-ragwe machanga huota baada ya siku Mbegu Inapendekezwa kutumia chotara aina ya F1. Aina hii ya mbegu imeonekana kuwa na mafani-kio makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na uwezo wa kumudu magonjwa.       Inapendekezwa kupata mbegu kutoka kwa wazalishaji walioidhin-ishwa.Aina za mbegu na uwezo wake?

Boston

Aina hii ya mbegu ina uwezo mkubwa wa uzalishaji. Wakati wa mvua aina hii ya mbegu husham-buliwa zaidi na magonjwa hasa ya ukungu.?
Serengeti: Aina hii ina uzalishaji wa wastani. Aina hii ina uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa.?

Tana:

 Aina hii uzalishaji wake ni mkubwa na wa muda mrefu. Inashambuliwa na magonjwa kwa wastani. Aina hii huhitaji kiwango kikubwa cha maji hasa wakati wa mavuno.Maharagwe machanga yamegawa-nyika katika makundi mawili;?
Maharagwe mateke kwa wastani (fine beans) na?Maharagwe mateke zaidi (extra fine beans)wataalamu walio karibu nawe.

  Epuka maharagwe kugusana na maji au tope wakati wa kuvuna kwani inaweza kusababisha ugonjwa wa kuvunda, hivyo kupata hasara.
Baada ya kuvuna weka kwenye chombo chenye matundu kwa ajili ya kupitisha hewa. Hii ni wakati wa kuvuna kutoka shambani. Baada ya hapo, maharagwe yawekwe kwenye kreti maalumu na kuwekwa sehemu yenye ubaridi kusubiria uchambuzi na kuwekwa kwenye madaraja pamoja na kufungashwa. 

   Endapo mbegu hazikuota vizuri unaweza kurudishia si zaidi ya siku mbili tangu maharagwe yaote.UmwagiliajiHii inategemeana na hali ya hewa/msimu, kulingana na eneo ulipo. Kwa kawaida maharagwe haya hustawi kwenye udongo usiotuamisha maji, na iwe kwenye ukanda wenye baridi ya wastani.
Utunzaji
 Inapendekezwa kuwasiliana na mtaal-amu wa kilimo alie karibu nawe baada ya siku 14 ili kufanya ukaguzi sham-bani kuona kama kuna dalili zozote za wadudu pamoja na magonjwa kama vile mnyauko fuzari, endapo kuna dalili zozote shauriana na mtaalamu.   Mkulima anaweza kutumia mbolea kwa ajili ya kukuzia na kurutubisha majani kulingana na mahitaji.  
Ni lazima kupanda mahindi kuzun-guka shamba la maharagwe ili kuzuia upepo unaoweza kuharibu maharagwe yako na yasiwe na ubora unaotakiwa.
Palizi Ni muhimu kufanya palizi kuanzia baada ya siku kumi ili kuepusha makazi/maficho ya wadudu wahari-bifu. Unaweza kunyunyiza dawa ya kuzuia kutu baada ya wiki tatu.  
Maharagwe machanga huchukua wiki 9-10 tangu kupanda hadi kuvuna. Hii inategemeana na hali ya hewa pamoja na mbegu.   Maharagwe haya huchanua baada ya wiki sita. Wakati  huu mkulima anatakiwa kuwa makini sana kutokana na uwezekano wa kuwepo wadudu waharibifu kama vile thiripi. Inapende-kezwa kuwasiliana kwa karibu na mta-alamu wa kilimo ili kufanya ukaguzi ili kubaini aina ya wadudu na hatua za kuchukua.
Uvunaji:

 Maharagwe machanga yanafaa kuvunwa viriba vinapokuwa na urefu wa sentimita 11.5-15, unene wa mil-imita 6-8. Hii hufanyika katika wiki ya 9-10. 

Kwa kuanzia, hapo juu ni maelezo mafupi juu ya kilimo hiki.

Share:

Blog Archive

Latest Posts

Translate

Popular Posts

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support